MWANAMITINDO wa Tanzania anayeishi Jiji la New York, Marekani, Flavian Matata, ameteuliwa kuwa balozi wa utalii nchini Marekani.
Uteuzi huo wa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Bodi ya Utalii nchini umekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua tangazo la vivutio vya utalii litalokuwa likirushwa na vyombo vya habari vya kimataifa ambavyo ni Shirika la Habari la Uingereza (BBC) pamoja na CNN.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Adelhelm Meru,
alisema baada ya kupata tangazo la kimataifa wameamua kupata pia balozi atakayesimamia shughuli za utalii
nchini Marekani.
Post a Comment