Unknown Unknown Author
Title: KIWANGO CHA STARS CHAWAFURAHISHA WADAU;MKWASA APIGIWA CHAPUO!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
...


Ile kaul iiliyowahi kutolewa miaka ya tisini na rais wa awamu ya pili ndugu Ally Hassan Mwinyi kuwa Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu sasa uwenda ikawa historia kwa taifa letu.
Ujasili huu nilionao wa kusema kuwa uwenda kauli hiyo itakuwa historia ni kutokana na kiwango kilicho onyeshwa na timu yetu ya taifa katika mechi ya kuwania kufuzu AFCON mwaka 2017 uko Gabon dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria.
Kama ilivyo ada kabla ya mchezo huo kulikuwa na maneno ya hapana pale kutoka kwa wadau wa soka wa hapa nchini kwa kila mmoja kusema lake.
Wapo waliosema Stars itabeba kapu la magoli kutoka kwa Nigeria lakini wengine walisema Stars ina nafasi ya kusahihisha makosa yake ya awali.
Ikumbukwe katika mechi yake ya kwanza Stars ilicheza ugenini na kulazwa kwa bao 3-0 kutoka kwa Misri.
Wakati wenzao Nigeria walishinda kwagoli 2-0 dhidi ya Chad hivyo kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kuelekea Gabon.
Waliosema Stars itabeba kapu la magoli walikuwa na hoja kuu mbili kwanza ni uimara wa timu ya Nigeria katika mashindano mbali mbali ya kimataifa.
Pili walilinganisha uwezo wa mchezaji mmoja mmoja katika kusakata kandanda na kuja na jibu la jumla kuwa Wachezaji wa Stars uwezo wao uko chini dhidi ya Nigeria hivyo ni lazima Stars wapigwetu.
Nao waliosema Stars ina nafasi ya kusahihisha makosa yao walikuwa na hoja ya uzalendo pekee ndani ya mioyo yao bila ya kueleza kiufundi jinsi gani Stars itapata uwezo wa kupambana na miamba Nigeria.
Wadau wote wa soka walisubiri kwa hamu kuona Stars itakuwa na utofauti gani na ile iliyo kuwa ikinolewana Marti Nooij ambayo ili vunja mioyo ya Watanzania kupenda timu yao.
KochaCharlse Boniface Mkwasa kwa kutazama uzito wa mechi hiyo aliipeleka timu nchini Uturuki katika mji wenye mwinuko wa Kartepe kwa kambi ya siku nane.
Siku hizo nane pekee zilitosha kuiandaa kifikra, kimbinu na pia kuiunganisha kiufundi timu nzima.
Ikiwa Uturuki Stars ilicheza mchezo mmoja wa kujipima ubavu na timu ya taifa ya Libya na kufungwa kwagoli 2-1.
Baada ya matokeo hayo Mkwasa alisema ameona upungufu wa timu yake na alisema atafanyia kazi upungufu huo uliojitokeza kabla ya mechi na Nigeria.
Siku ya mechi na Nigeria wote tumeshuhudia mabadiliko ya kiuchezaji ya timu yetu kuanzia kwenye ulinzi kwenye viungo na kwa washambuliaji.
Tukianzia kwenye nafasi ya ulinzi, golikipa alisimama Ali Mustapha mabeki walicheza vizuri sana bila yapapara yoyote, safu hiyo iliundwana Hajji Mwinyi Mgwali, Shomari Kapombe, Kevin Yondani na Nadir Haroub “Cannavaro” ambapo waliwabana vilivyo Washambuliaji wa Wanigeria.
Safu ya kiungo iliundwa na Himid Mao, Farid Mussa ambae alicheza kwa kiwango cha juu kabisa na kuonyesha n ichaguo sahihi, mwingine aliyecheza katika nafasi hiyo ya kiungoni MudathirYahya.
Katika eneo hili viungo wawili walikuwa na jukumu la kukabana mmoja akipandisha mashambulizi, jukumu hilo alipewa kijana mdogo kabisa FaridMussa.
Ambaea litimiza kwa uzuri majukumu hayo na kutusaulisha kazi ya Simon Msuva mfungaji bora wa ligi kuu msimu uliopita.
Kwa mbinu ya kutumia viungo wawali wakabaji Mkwasa alifanikiwa sana kuzima ndoto ya Nigeria ya kuchukua pointi tatu ugenini.
Kwa upande waushambuliaji uko ndiko utamu wa Stars ulinoga sana, utamu huo ulichagizwa na ubora wa Mbwana Ali Samatta, Thomas Ulimwengu bila kumsahau Mrisho Ngassa “Anko” baada ya mechi hiyo kila Mtanzania ameonyesha kufurahiswa na uwezo wa timu yetu.
Kwa ubora ule wa Stars sioni sababu za kumnyima mkataba kocha Charles Boniface Mkwasa kuendelea kuitumikia taifa Stars.
Mkwasa ana kaimu nafasi ya kocha mkuu baada ya aliyekuwa kocha mkuu Marti Nooji kuvulunda kwamechi 11 bila kupata ushindi uku vipingo 5 mfululizo vikifanya kocha huyo aondolewe.
Ndipo rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi akampa nafasi hiyo Mkwasa kuikaimu kwa muda wa miezi mitatu kuanzia mweziJulai.
Siku zina kwenda mbio kweli lakini bado TFF iko kimya juu ya mustakabali wa kocha Mkwasa kama ana endelea na ukocha mkuu au ana kuja kocha mwingine.
Mimi nafikiri Mkwasa ndio ana paswa kupewa nafasi hiyo na kuaminiwa na Watanzania pamoja na TFF hili kazi yake ifanikiwe.
IMEANDIKWA NA VICTOR SIMON WA KWANZA-JAMII RADIO

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top