Unknown Unknown Author
Title: MWENYEKITI UVCCM ROMBO ATANGAZA KUMUNGA MKONO LOWASSA,AJITOA CCM!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jinamizi la kukimbiwa na wanachama limezidi kukiandama Chama Cha Mapinduzi, baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vij...
Jinamizi la kukimbiwa na wanachama limezidi kukiandama Chama Cha Mapinduzi, baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Beatrce Shirima, kujiuzulu wadhifa wake baada ya kutuhumiwa ana muunga mkono mgombea urais aliyesimamishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chadema, Edward Lowassa.

Beatrice amefikia uamuzi huo ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro, Fredy Mushi na Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM mkoani hapa, Paul Matemu kujiunga na CHADEMA.

Akitangaza uamuzi huo jana, Beatrice alisema kwa kipindi kirefu amekuwa akinyimwa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa CCM kutokana na kile anachodaiwa kuwa, yeye ni mmoja wa waliokuwa wanamuunga mkono Lowassa.

“Nadaiwa kwamba nina kisaliti chama na kuwasaidia Ukawa katika kampeni zao. Siyo jambo la kweli na sijawahi kuhusika katika kuwapigia kampeni CHADEMA,” alisema.

Alisema ameamua kujiuzulu nafasi hiyo na kujivua uanachama wa CCM bila ya kushinikizwa na mtu yeyote, kwa kuwa ni maamuzi yake binafsi.

“Nimeamua kujiweka pembeni na nimejitoa CCM; Mimi sio kiongozi tena wa vijana na maamuzi haya sijashauriwa na mtu yeyote bali ni maamuzi yangu binafsi” alisema.

Chanzo: Nipashe

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top