SITTA;BUNGE LA KATIBA LINA MAMLAKA MAKUBWA KULIKO TUME YA WARIOBA!
Baada ya watu na taasisi kadhaa kudai kitendo cha Bunge Maalumu la Katiba kupokea maoni ya wananchi na kuyaongeza kwenye rasimu ya Katiba mpya, ni kuingilia kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta, alisema bunge hilo lina mamlaka makubwa kuliko tume hiyo.
Amesema hata wajumbe wa bunge hilo wanaoendelea kupitia rasimu hiyo, siyo mazuzu, wana akili zao, wasomi na wapo watu wengi wanaotambua kazi hiyo na kuipongeza.
Sitta alivunja ukimya huo na kutoa ufafanuzi jana mbele ya
waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, na kuongeza kuwa wananchi wameona rasimu ya Katiba mpya, ina upungufu.
“Mimi naelewa kuna watu wanakasirishwa sana na kazi tunayoendelea kuifanya, ni haki yao kukasirika lakini kinachofanywa ni wananchi ambao hatukuwaalika, wanakuja kwa makundi kuelezea wanachoona kuwa ni upungufu ndani ya rasimu, sasa haya watayapeleka wapi?
“Hii hali ya kuonekana sisi Bunge na Tume tupo hadhi moja si kweli, Tume ina mamlaka yake lakini Bunge lina mamlaka makubwa zaidi ya Tume… waliotunga sheria waliona ipo kazi inayofanyika pamoja na kufanya marekebisho ndio maana wanachotoa wao ni rasimu sisi tutakachotoa inaitwa Katiba inayopendekezwa.”
Alisema dhana kwamba lolote likifanywa kwenye rasimu ni usaliti kwa nchi au inachakachuliwa, msingi wake ni ghadhabu za mtu na uamuzi tu wa kuwaona waliopo Dodoma ni mazuzu.
“Hapa kuna watu wasomi wazuri tu wenye akili zao. Kusema tunafanya kazi ya Tume ni upotoshaji mwingine wa watu wasiotakia mema Bunge Maalumu la Katiba. Sijui kwa nini rasimu inapewa hadhi kama msahafu, wakati imeandikwa na binadamu tu ina upungufu mkubwa.
sitta
29
Aug
2014
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.