Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kuwataarifu wananchi na abiria waliokuwa wasafiri na treni ya leo Ijumaa Julai 24, 2015 kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho saa 11 jioni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea leo Ijumaa Julai 24, 2015 saa 8:15 alasiri maeneo ya Stesheni za Mazimbu.
–Mkata mkoani Morogoro ambapo ilihusisha mabehewa matano ya treni ya mizigo iliyokuwa inasafiri kwenda Bara, manne yaliacha njia na moja kuanguka kabisa.
Tayari Wahandisi wa TRL wako eneo la ajali kufanya tathmini na kuanza zoezi la uokoaji, ikiwemo kazi ya kuyanyanyua mabehewa yaliyopata ajali na kisha kukarabati njia ili iwezwe kupitika mapema hapo kesho.
Uongozi wa TRL inawaomba radhi wananchi na wateja wake wote nchini kwa usumbufu utakaojitokeza.
-Tamati-
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Elias Mshana
Dar es Salaam,
Post a Comment