Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale ambapo Sir Chande, kiongozi mstaafu wa taasisi hiyo Afrika Mashariki alipokuwa akishukuru kupewa heshima na vyombo vya kitaifa na kimataifa.
Baadhi ya vitabu vinaonesha kwamba hakuna anayejua wanachokifanya wanachama wa Freemasonry lakini inaaminika kuwa viongozi wakuu wa Tanzania wanajua kila kitu.
SASA ENDELEA…
Katika zama tulizo nazo swali la nani ni Freemason limezoeleka. Hapana shaka kila mtu anaweza kuwa na baba, mama, babu, bibi, mjomba au binamu lakini Freemasons ni kundi la udugu mkubwa duniani na la zamani la watu waliojipambanua.
Kama ilivyo kundi la akina mama, kundi hili linaweza kuwa la madaktari, wafanyakazi wa benki, viwandani au walimu.
Kwa Wagiriki wa zamani, Freemasons walikuwa ni wasomi na wanafunzi wa vyuo vikuu.
Freemasons ni watu waliojiunga pamoja kwa sababu kuna mambo au vitu wanavyotaka kuvifanya ndani ya fikra zao. Jamaa hawa hupenda kuwa karibu mno na watu wanaoheshimika na hueshimiana nao.
Bado baadhi ya vitabu vinaonesha kuna mkanganyiko wa asili ya Freemasonry. Kuna uwezekano Freemasons walishawishiwa na mashujaa wa kidini waliokuwa kwenye kundi la kitawa la Kikristo lililoundwa mwaka 1118 kusaidia kuwalinda waliokuwa wakienda kusali katika nchi takatifu.
Jumba Kubwa (Grand Lodge) ambayo hata hapa kwenye ipo Posta jijini Dar ndiko walikokuwa wakikutania. Hii ni sehemu yenye mamlaka ya kuongoza maeneo fulani ya Freemasons.
Nchini Marekani kuna nyumba hizi kubwa za kukutania katika Jimbo la Columbia. Nchini Canada nako kuna majumba haya katika kila mkoa. Si hivyo tu, pia kuna sehemu za kukutania katika kila mji na katika miji mikubwa kwa kawaida ziko kadhaa. Nchini Marekani kuna sehemu kama hizo zipatazo 13,200.
Kwa mujibu wa Freemasons, wenyewe ni taasisi ya kipekee inayojihusisha na sehemu kubwa ya maisha ya kijamii nchini Marekani kwa zaidi ya miaka mia mbili na hamsini (250) iliyopita.
Wanadai ni jumuiya yenye udugu mkubwa wa zamani na unaoendelea kuwa sehemu muhimu ya maisha binafsi ya watu na makuzi yao.
Wanasema ni taasisi ya watu waliofungamanishwa na filosofia ya mafundisho na uelewa wa kawaida na udugu unaowafanya watu wote kuwa sawa.Freemasons ni watu walioamua kwamba wanapenda kujiona na kujisikia bukheri wa afya kwao wenyewe na wengine. Hujali sana kuangalia kitu gani kitatokea siku za usoni na hata wakati uliopita na kufanya kila wawezalo ama mtu akiwa peke yake au na wengine. Ishu kwao ni kuufanya wakati ujao kuwa mwema kwa kila mmoja.
Kwa mujibu wa Mchungaji Joseph Fort Newton, mtumishi wa Mungu na mchungaji mkuu aliyejulikana sana katika nusu ya kwanza ya karne ya 20 aliyekuwa katika Jumba Kubwa la Iowa, kati ya mwaka 1911-1913, Freemasons si dini, lakini imeweka msisitizo mkubwa katika Umungu Baba na kuhakikisha kuwa udugu wa kibinadamu unafuata misingi ileile ya Umungu Baba.
Hii ikiwa ni pamoja na wajibu wa utekelezaji wa kile kilichoitwa Golden Rule yenye lengo la kujenga jamii moja yenye nguvu sana. Ukibahatika kukutana na Freemasons, tarajia kuwa utakirimiwa kadiri utakavyopenda kukirimiwa. Lengo hapa ni kukuhudumia ili uwe kama mshiriki wa Michigan, Marekani kwenye jumba lao la kukutania la Michigan ili uwe chanzo cha habari zinazowahusu Freemasons na wasio Freemasons kwa pamoja wa Jimbo la Michigan na wengineo duniani.
Unawezaje
kuwa miongoni mwa Freemasons endapo tu utapata fursa ya kutupa jicho kupita mabonde na milima hadi mwisho wa upeo kwa fikra iliyozama na kujiona udogo wako mbele ya Mungu huku ukiwa na imani ya dini, matumaini na ushujaa ambavyo ndiyo mzizi wa kila uadilifu.
Wakati miti na mimea mingine maarufu ikimetemeta katika miale ya jua kwenye maji, ikitulia kama vile mawazo ya mtu aliyependwa sana aliyekufa muda mrefu uliopita, Freemasons kazi yao ni kumsaidia mtu anayelia kwa huzuni.
Wakati hakuna sauti za kilio cha huzuni zinazosikika masikioni mwao, mikono yao huwa haitoi msaada bila kuwa na majibu.
Watakapoona jambo jema katika kila imani watamsaidia mtu yeyote kuleta msaada wa kiungu na kuiona maana tukufu za maisha bila kujali imani hiyo inaitwaje.
Watakapoweza kuangalia kidimbwi cha maji njiani na kuangalia ndani zaidi ya kidimbwi hicho na kuangalia uso usio na matumaini wa mtu anayekaribia kufa na kuona kitu kilichojaa dhambi ndipo hujitoa kusaidia.
Watakapojua jinsi ya kusali, jinsi ya kupenda na jinsi ya kuwa na matumaini, watakapokuwa wanajiamini wao wenyewe na kuwa na imani na wenzao na Mungu wao huku mikononi wakiwa wameshika upanga wa ubaya, ndani ya mioyo yao wakiimba nina furaha ya kuishi lakini naogopa kufa.
Usikose kila Jumatano kwenye Gazeti hili la Risasi Mchanganyiko. Kwa maoni tuwasiliane kwa namba hiyo hapo juu.
Post a Comment