MJUMBE DARASA:Umewahi kujiuliza kwa nini mara nyingi ni vigumu kuelewa na kaka au dada yako?
Ndugu Watanzania ningependa kushare nanyi kuhusu utafiti wangu mdogo nilioufanya katika familia nyingi za Kibongo na hata duniani kote kuhusiana na hili nililolileta kwenu siku ya leo.Wakati wengine wakiendelea kufurahia mahusiano ya kifamilia, kwa upande mwingine hali imekua tofauti kwa baadhi yetu wengine,dada au kaka ndo wamekua adui wakubwa na hakuna maelewano hata katika vitu vidogo tu kama vile mali, kuingia chumbani kwa dada au kaka yako bila kubisha hodi,kuvaliana nguo,kujaribu kuwa kiongozi wa familia, na sababu nyingine kibao.
Katika kutafuta maoni kwa wadau nimeona sio mbaya nikiwaleta watanzania karibu na hili ili kuweza kuboresha mahusiano ya washiriki katika familia zetu.Ninachoamini mimi, uwezo wa mtu kuishi vizuri na jamii unategemea sana na jinsi anavyoishi nyumbani na anavyodeal na ndugu pale pale home.Kuna msemo wa kiswahili unaosema "Ishi na watu uvae kiatu";Tafsiri ya maneno haya ni kuwa mahusiano mazuri na wengine ni chachu ya mafanikio ya maisha hasa ukizingatia kizazi chetu cha sasa chenye kila aina ya changamoto za kimaisha.Katika matukio mengi yanayosababishwa na mahusiano mabaya baina ya ndugu (dada,kaka na ndugu wa karibu) yameleta madhara makubwa kwa familia na jamii kiujumla kwani mengine yamepelekea kufikia hadi kuuana kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia kuhusu mali na vitu vingine.Ningeomba kama familia na jamii yote kwa ujumla tujaribu kutafuta njia ya kutatua matatizo madogo ya baina ya ndugu,dada au kaka katika familia ili kila mmoja wetu aweze kufurahia maisha na kujamiiana vizuri ndani ya familia na nje pia.
Na Mjumbe jr
Dar es Salaam
Post a Comment