Unknown Unknown Author
Title: PICHA ZA AJALI NA TAARIFA KAMILI YA AJALI YA MWIMBAJI WA INJILI BAHATI BUKUKU HIZI HAPA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
gari aliyo kuwemo Bahati Bukuku na Wenzake Bahati Bukuku akiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kongwa Bahati Bukuku akiwa kwenye hospitali ya...
gari aliyo kuwemo Bahati Bukuku na Wenzake
Bahati Bukuku akiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kongwa Bahati Bukuku akiwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Kongwa. Usiku wa kuamkia leo, muimbaji nyota wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku pamoja na wasaidizi wake, walipata ajali akiwa njiani kuelea Kahama kwenye huduma. GK ilikuripotia taarifa za awali, na hapa tunakuletea pcha kamili na taarifa rasmi ya jeshi la polisi mkoani Dodoma. Juhudi za kumhamishia Bahati Bukuku kuelekea Muhimbili kama ilivyopangwa awali zimeshindikana, kutokana na kushindwa kugeuka wala kuinuka - akiwa amelazwa. Tayari ndugu na marafiki walishafika kutoka Dar es Salaam, na watu kadhaa wa Dodoma na viunga vyake walipita kuwajulia hali na kuwafariji. Taarifa ya Jeshi la Polisi, Dodoma. Gari lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU (31) mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine linalosadikiwa kuwa Fuso. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 saa tisa alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa. Waliojeruhiwa ni EDSON MWAKABUNGU ambae analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI BUKUKU (40) ambae ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake. Mwingine ni FRANK CHRISTOPHER (20) mwimbaji pia wa nyimbo za injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam ambapo kapata michubuko usoni na mkono wa kulia. Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri ambapo Kamanda Misime amesema walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili. Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.
Rafiki yake Bahati Bukuku Jennifer Mgeni akimjululia Hali mwenzake Picha zote kwa hisani ya Alpha, ambayealitoka bila kuwa na majeraha kwenye ajali hiyo, wakati dereva, Eddy (Edson Mwakabungu) yeye ameripotiwa kuwa mguu umevimba, kiasi cha kulazimika kutoa jeans aliyokuwa amevaa. Credit:GK

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top