Picha haihusiani na tukio.
Jamani Tanga hali si shwari.Muda huu Rais
ameshatoa kibali cha kwa JESHI LA WANANCHI
WA TANZANIA( JWTZ) kupambana na magaidi
waliojificha mapangoni baada ya jeshi la polisi
kushindwa kupambana na magaidi hao.
Taarifa nilizopewa na mwanajeshi kutoka Jeshi la
Wananchi( JWTZ) ambaye ni CLACMATE wangu
Wa kantalamba sekondari na mwingine CLACMATE
wangu wa Ileje sekondari ni kwamba Jeshi la
Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) limeshaanza
kurusha mizinga kuelekea mapangoni na hata
wanajeshi wenyewe wanaogopa kuingia mapangoni
moja kwa moja kwani magaidi hao inaonekama
wana vifaa vya kisasa vya kivita.
Mimi Nitaondoka Tanga kuelekea Dar es Salaam
maana mpaka sasa tayari polisi wanaanda Taarifa
ya umma kupiga marufuku mikutano na
mikusanyiko ya Wananchi.
Hizi ni taarifa kutoka kwa wanajeshi ambao wako
Field na wanapata taarifa .Tusubiri.
Na Daniel Ezekiel Daniel
MAELEZO ZAIDI:
Wadau naomba sasa niwape ukweli wa kinachojiri Tanga kuhusu sakata la Al Shabab.
Yapata wiki moja Polisi walimkamata mtuhumiwa mmoja anajulikana kwa jina la Master ambae inasemekana ndiye aliyekuwa akiratibu uporaji wa silaha vituo vya polisi na polisi wenyewe. Matukio haya yametokea kule Ikwiriri Rufiji Pwani baada ya kituo kuvamiwa na Tanga Chumbageni kwa askari kuporwa silaha wakiwa katika doria.
Katika kutumia weledi wao wa kupata habari, ililazimika sasa polisi waende eneo ambalo mtuhumiwa anasema ndiko silaha wanazopora zilipofichwa. Alieleza silaha wanaficha maeneo ya Amboni ambako Wachina waliojenga barabara ya Horohoro waliweka kambi. Kwa hiyo magaidi hayo hayapo mapango ya Amboni tunayoyafahamu.
Baada ya kufika eneo la tukio mtuhumiwa akiwa na pingu alijirusha kwenye pango hilo huku polisi wakiwa wanashangaa nini kimetokea. Ikumbukwe mtuhumiwa huyo alikuwa na pingu. Baada ya mtuhumiwa tu kutua chini au kiliposikika kishindo basi haikupita muda mvua ya risasi ilianza kunyesha kuelekea polisi walipo pamoja na mabomu ya kurusha kwa mikono. Bomu mojawapo lilifanikiwa kumjeruhi askari polisi mmoja ambaye ameshonwa nyuzi kama kumi na moja hivi. Kwa hiyo hakuna polisi aliyekufa kwenye tukio hilo.
Baada ya kuona hali imekuwa ngumu ilibidi OCD aliyekwenda kwenye tukio kuomba msaada zaidi kwa FFU Tanga. Napo hali ikawa tete, ndipo ilipolazimu kuomba msaada kutoja Jeshi la Wananchi Tanzania.
Kama uelewevyo kuomba Jeshi la Wananchi kuingilia kati na lazima CDF atoe kibali na ithibitike kuna ulazima.
Hatimaye saa tisa za mchana kibali kilipataka na Jeshi la Wananchi kwenda eneo la tukio. Walipofika waliona kuna ulazima wa kutumia silaha nzito ili kulifumua pango hilo ambalo ili kujua kilichopo. Kuanzia hapo mizinga imekuwa ikisikika maeneo hayo ishara ya kwamba wanaume wapo kazini.
Katika kuongeza nguvu kikosi maalumu kimeongezwa kutoka Dar ili kuhakikisha hali inakuwa salama.
Hadi leo asubuhi bado mizinga ilikuwa ikisikika licha ya kwamba saizi haisikiki tena.
Lengo la hao Al Shabab inasadikiwa ni kutoka kuwakomboa wenzao ambao wamefungwa au wapo Magerezani. Kwa mantiki hiyo, sakata kubwa lipo katika ulinzi wa Magereza ambapo wanasema ni wakati wa kulipa kisasi makubwa ambayo waliyataja ni Gereza Lilungu lililopo Mtwara, Gereza Arusha na Gereza Segerea lililopo Dar.
Pamoja na hayo bado ukweli unabaki wazi wanaweza kuvamia gereza lolote ili kutimiza malengo yao.
Ni jukumu sasa la vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha hali haiwi alijojo.
Mungu Ibariki Tanzania.
MJUMBE BLOG
Tuta kuletea taarifa mpyq kila zinapo kuwa zinatufikia.
Hajaaa
Jajaaka
Jaajajsi
tulikua shule galanos na mambo yalikuwa sio shwar, milio yote tulikuwa tunaiskia...usiku wake kila m2 hakulala mpaka asubuhi
ReplyDelete