Unknown Unknown Author
Title: HADIDU ZA REJEA:KUHUSU USALAMA WA WATOTO KATIKA MSIMU WOTE WA SIKUKUU!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
ENEO LA MAREJEO:Mji Mdogo wa Mlowo-Mbeya NINI:Usalama wa Watot LINI:Krismas na Mwaka mpya Kwa Ndugu,jamaa na Marafiki; Kwanza kabisa...

ENEO LA MAREJEO:Mji Mdogo wa Mlowo-Mbeya
NINI:Usalama wa Watot
LINI:Krismas na Mwaka mpya

Kwa Ndugu,jamaa na Marafiki;
Kwanza kabisa nina penda kuwa takia Kheri na Fanaka tele kuingia Mwaka 2014! Tulio uanza Rasimi.... Mimi nasema baada ya yote yaliyo pita 'Maisha ni lazima yaendelee',Hakuna sababu ya kujutia matunda ya machaguo yetu,cha msingi tuyakubali na tusonge mbele.
Baada ya kufanya upembuzi wa kina katiak misimu yote ya sikukuu zilizo pita kuna wazo  nilikutana nalo na Nikaona kama ni vema nikaliweka Ukutani/kwenye Ukurasa wangu ili wadau nao walipime wenyewe.Nikiwa Mbeya-Mlowo nilikutana na jambo ambalo ni kama Utamaduni ulio jijenga kutokana na hulka ya mazoea kwa wenyeji ama ni kusahau wajibu wetu au kupuuza na kusubiri mpaka majanga yatokee ndipo waanzishe harakati(kwani wa Tanzania kwa kawaida huendeshwa na matukio na sio mfumo) za kuwa kamata walezi,wazazi na wasababishi wa janga ili wawajibike.Lakini nivema ikumbukwe kuwa KINGA NI BORA KULIKO TIBA.
   Watoto kama walivyo kutwa na Mpiga Picha Wetu

USALAMA WA WATOTO KATIKA KIPINDI CHOTE CHA SIKUKUU;Umekuwa finyu mno kiasi cha kuhatarisha uhai wao,Suala ambalo kwa sisi tunao amini katika miujiza tuna weza kusema ni MUNGU ame wanusuru watoto wetu wasipatwe na ajari katika Msimu wote wa Sikukuu.Baadhi ya mambo niliyo shuhudia:-
1.Watoto kuachiwa hovyo bila uangalizi wowote wakusanyike Bara barani na kuanza kucheza michezo ya kufukuzana,huku wengine wakiripua baruti na pembeni kidogotu ya bara bara kuna akina mama wana endelea kuuza juisi,Barafu,Vitumbua,Maparachichi,maembe,Ice cream bila wasi wasi na Magari,Pikipiki,Baiskeli ziki endelea kutumia barabara hiyo na kupishana kwa kasi bila tahadhari yoyote kuchukuliwa na wahusika wa pande zote.Tukio hili nililishuhudia Siku ya Kris Mas na Mwaka mpya,Bara bara iendayo kamsamaba-Mkabala na Duka la Mahenge Upande wa Soko kuu Mji mdogo wa Mlowo,Mita Chache tu kutoka Transfoma ya TANESCO ilipo.

   Mbele Pichani ni Umati wa Watoto wakiendelea kucheza Bara barani na Magari yakipita kasi

2.Watoto kuachiwa wazurule hovyo usiku kucha kwa kisingizio cha Mkesha(Mwaka mpya na Krismas);Kwa uelewa wangu finyu na exposure ndogo niliyo nayo mimi nime ona  katika miji mikubwa kuna utaratibu wa watoto kufanyiwa Disko Toto,Mida ya Mchana Kweupe kwa uangalizi maalum na muda maalum.Tofauti na Mlowo ambapo kelele,Filimbi,Ngoma,madebe na vuvuzela hupigwa usiku kucha huku kundi kubwa la watoto liki katiza mitaani na Barabarani(Barabara kuu Tunduma-Dar) na Wengine kukaa pembezoni mwa Barabara huku wakicheza,Wangine walionekana Upenuni mwa Vilabu vya pombe(Bar&Guets) wakizurula bila Tahadhari za Kimaadili wala kiusalama kuchukulia na upande wowote.Hili ni Tatizo,Kama wahusika walikuwa hawajui nivema wakajulishwa ili Msimu mwingine wa Sikukuu haya yasi jirudie.

  Wototo Wakiwa Barabarani Mlowo(Dar-Tunduma);Bila Uangalizi kama walivyo kutwa na Mpiga Picha wetu Usiku wa Mkesha.

HITIMISHO:Ulinzi na Usalama wa Watoto wetu ni jumkumu la jamii nzima "Mtoto anahaki ya kucheza,Kweli! Lakini Tukumbuke kwamba;Uhuru usio na mipaka ni Vurugu.
Rai yangu kwa wazazi na Uongozi kwa ujumla,Nivema kama Tahadhari za Kimaadili na kiusalama zika chukuliwa mapema,hasa kuanzia makanisani zinako fanyika misa takatifu kwa wazazi na walezi kukumbushwa kuwa makini kwa watoto wao ili Haya yasijirudie na yakaja kusababisha maafa siku zijazo.Mimi Sio mtabiri! Lakini Nisinge penda yatokee ya kutokea ndio tukumbuke.


ZINGATIO:Tahadhari hii iwafike wote sio Kwa Mlowo tu,Mlowo ni kama Eneo la Mfano tu,Naomba Msije mkani nukuu Tofauti.
Nakala kwa uongozi wa kijiji

Elasto Mbella
Mbeya/Mlowo
0752025002

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top