Huku baadhi ya Mashabiki na Wachezaji wakiwa hawa amini wanacho kiona,Mpira ulimalizika kwa Timu ya Mpakani ama Leopard kama wanavyo jiita wao Kuibuka na Ushindi mnono kwa kuwa mbele kwa Magoli Mawili kwa Moja Zidi ya Washindani wenzao Yamaha.
Pichani ni Mashambulizi Mita Chache tu,Toka Lango la Leopard
Shangwe ndelemo,Tambo,Majigambo na Vifijo vilizizima kwa muda ndani ya uwanja wa shule ya Msingi Msense! Zikifuatiwa na Hafla fupi ya kukabidhiwa zawadi kwa baadhi ya Washindi na Washiriki wa MSYETE CUP waliokuwepo katika Viwanja hivyo.
Sehemu ya Umati ya Walio jitokeza Kushuhudia Fainali za MSYETE CUP
Mgeni Rasimi Ndg.Abraham Msyete Akisimama Ili kutoa Utambulisho kwa viongozi na wadau wa Ligi.
Utambulisho kwa baadi ya viongozi ya ngazi ya Wilaya Ulianza;Baada ya wenyeji kujitamburisha kama ishara ya kuwa Karimu wageni wao.
Makamu Katibu chama cha Mpira wilaya Ndugu Kasebele akiupungia mkono umati Ulio hudhuria
Ndugu Aroni Sinka;Mwenyeji wa Ugeni ulio hudhuria
Ndugu Samahani Mwasote;Akisisitiza jambo kwa umati
Shangwe zililipuka baada ya Kumsimamisha Kijana wake Martin;Na Kusema amewaletea Watoto wanao cheza Mpira Zawadi pia!
Ndg Abraham Msyete;Akijitambulisha Rasimi kwa Umati Ulio Hudhuria
Hapa ali pata fursa ya kueleza baadhi ya mambo aliyo yaona kama changamoto katika Ligi;Suala la Mafunzo kwa Marefalii ambalo lilionekana kumugusa kila mwana michezo aliye kuwepo uwanjani hapo,Pia Ali sema 'Inatupasa kuyaendeleza haya yaliyo mema ndani ya jamii yetu.. ' Huku akizisifu timu zote zilizo shiriki ligi hiyo,Aliwapongeza sana Washindi wa pili na Wakwanza ka kuonesha ushindani wa hali ya juu katika kipindi chote na hata Kufikia kumpata mshinindi.
Mchezaji Bora akichukuliwa Zawadi kwa Niaba na Kiongozi wake Tsh,10000/-
Mfungaji Bora Ndg Seward Isega Akikumbatiwa na Mgeni Rasimi kama Ishara ya Pongezi
Kamati Tendaji Iliyo Fanikisha Ligi na kuifanya ifane Ilipokea zawadi zao Pia!
Mshindi wa Tatu Iwindi Akipita Mbele kukabidhiwa Mpira na Tsh.10000
Mshindi wa Pili:Yamaha Akinyakua Jazi pea moja,Mpira na Tsh.150000/=
Mshindi wa Kwanza:Leopard/Mpakani! Akijinyakulia Jezi pea Moja,Mipira 2 na Tsh.200000
Picha ya Pamoja ya Kumbukumbu ya Ligi ya "MSYETE CUP"
Zoezi la ugawaji zawadi lilifuatiwa na Kupiga picha ya Pamoja kwa wachezaji wa Timu zote mbili.Leopard na Yamaha.
Pichani:Baadhi ya Wachezaji wakiwa ndani ya Uzi Mpya na Nyuso Zenye Furaha tele
Martini Abraham Msyete;Akiwakabidhi watoto wenzake Zawadi ya Mipira miwili(Kama Baba,Kama Mwana).
Refarii akiteta jambo na warusha kibendera
Pichani juu kabisa ni Benchi la Rizevu la Timu ya Yamaha;Na Timu ya Leopard Picha ya chini
Leopard/Mpakani waki rudi na Ushindi wao! Huku Bendera ya timu yao ikipepea
Baadhi ya Ugeni ukichukua nafasi ili Kuanza Safari Tokea viwanja vya Shule ya Msense.
Mpaka Kamera yetu ina ondoka eneo la Shule ya msingi Msense,Isansa Utulivu na Amani kwa wadau woet wa michezo vilitawala.
Shukrani za Pekee ziwafikie Wadau walio;Tuma Usafiri Kumchukua Mpiga picha wetu Eneo Alipo Haribikiwa Usafiri wake ili afike kwa wakati na asikose kwenye Tukio zima la Fainali hiyo!
MJUMBE BLOG;Tuna amini nawe umefaidi uhondo kwa kushiriki Kutazama baadhi ya matukio nyeti yaliyo jili kwenye Ligi ya "MSYETE CUP".
Asante kwa Kuendelea kutupa Ridhaa Tukuhudumie!
#@Kheri ya 2014!
MJUMBE sr
Post a Comment