Unknown Unknown Author
Title: JAMES ZOTTO NA WAZO LA SERIKARI TATU :TATIZO LETU WASOMI WA NCHI HII TUME VUTWA SANA NA MIHEMKO YA VYAMA TUNAVYO VISHABIKIA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
James Zotto Yesterday near Dar es Salam JK achukue tahadhari: Mimi ninatambua, serikali yoyote ipo strategist zaidi.Kuvunjw...
JK achukue tahadhari: Mimi ninatambua, serikali yoyote ipo strategist zaidi.Kuvunjwa kwa katiba ile juzi si suala ambalo halikupangwa.Lilipangwa.Lengo limetimia.Na sababu eti, wajumbe wangekaa muda mrefu na gharama kubwa kuwaweka Dodoma ni hoja dhaifu sana.Gharama iko wapi kwenye kusimamia misingi ya nchi?Iko wapi katika kupata katiba?Gharama ipi hasa wakati zimetumika na bado zinatumika?Hoja ya kipuuzi kabisa.Na tatizo letu wasomi wa nchi hii tumevutwa sana na mihemuko ya vyama tunavyovishabikia hata kama vinapotoka.Jamani, Chama cha Siasa ama Serikali si kama timu ya mpira! Ndo maana unaweza ukaona maprofesa ama wanasheria nguli wakitetea uharo tena bila kujali wanajiaibisha linapokuja suala la Chama chake! Wasomi tumewasaliti wananchi wa nchi hii. Ule mchezo wa juzi ulilenga kuwa Warioba aseme alafu waone mapungufu na yaliyo na hoja nzito, ili Mkuu wa kaya aje na msimamo(nafikiri wa chama chetu) na aonyeshe tunataka serikali ngapi!Asemacho yeye ndicho kitakachopita!Si wamesema kuwa Wajumbe wanamamlaka ya kubadilisha vifungu badala ya kuviboresha tu!Injinia wa spidi na Viwango pamoja sisi wa Kijani tunataka vidole viwili!Jipya liko wapi?

JK achukue tahadhari.Aliunda kamati na hakuwaambia anataka katiba ya aina gani.Bali aliwaambia wakusanye maoni na walete Rasimu.Baada ya rasimu kuletwa, kumbe tulitaka serikali mbili.Kunahaja gani ya kupoteza muda wote huo na mipesa kibao? Endapo JK atasema lazima serikali mbili, basi itaonekana hakuwa na nia ya maoni na kuwa hayupo kupata maoni mbadala(si tofauti). Endapo atasema serikali tatu, ajue atawakwaza waachama wake sisi ambao ni kundi dogo linalotaka serikali mbili.Swali, je, atatii maoni ya wengi?Atasaliti maamuzi yake mwenyewe? Utashi wahitajika sana.Hapa haihitajiki siasa, ni ukweli na uwazi.

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top