Unknown Unknown Author
Title: LIGI YA MABINGWA 2013-2014:TUMAINI LA MWISHO KWA MANCHESTER UNITED
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  London, England Manchester United, ambayo msimu huu inaonekana kupoteza nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, wiki hii itaa...


 London, England
Manchester United, ambayo msimu huu inaonekana kupoteza nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, wiki hii itaanza kutupa kara zake za mwisho kwenye michuano hiyo wakati wa mechi za robo fainali zitakazochezwa kesho na keshokutwa kabla ya mechi za marudiano zitakazochezwa Aprili 8 na 9.
Karata hizo za Man U ni ngumu kutokana na ukweli kuwa inakutana na Bayern Munich kwenye Uwanja wa Old Trafford kabla ya kumaliza raundi hiyo kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Katika mechi nyingine Barcelona itaikaribisha Atletico Madrid kwenye Uwanja wa Camp Nou, Hispania.
Man United vs Bayern Munich
Mechi ya Man U na Bayern ni kumbukumbu ya fainali za mwaka 1999 ya Ligi ya Ulaya wakati Manchester iliposawazisha katika dakika ya mwisho na kufunga bao la pili lililoipa klabu hiyo kongwe ya Uloaya ubingwa wa pili wa Ulaya kwa kushinda kwa mabao 2-1.
Bayern Munich ilipata bao la kuongoza mapema katika dakika ya 6 lililofungwa na Mario Basler, lakini Manchester ilisawazisha dakika ya 90 kwa bao la Teddy Sheringham na kuongeza bao la pili dakika ya tatu ya majeruhi lililofungwa na Ole Gunnar Solskjaer.
Hata hivyo, katika mipambano mingine ya timu hizo katika hatua ya robo fainali msimu wa 2009/10 na 2000/01,  Bayern iliibuka kidedea.
Barcelona vs Atletico Madrid
Barcelona itakutana na vinara wa Ligi Kuu ya Hispania Atletico. Licha ya timu hizo kukutana mara kwa mara katika La Liga, hii itakuwa mara ya kwanza kukutana katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Keshokutwa pia Real Madrid itaendelea kusaka taji lake la 10 la ubingwa wa Ulaya itakapoikaribisha Borussia Dortmund kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, huku  Paris Saint-Germain ikiumana na Chelsea kwenye Uwanja wa Parc des Princes.
Real Madrid vs Dortmund
Msimu uliopita Bayern na Dortmund zilikutana katika nusu fainali na Dortmund ilishinda mabao 4-1 nyumbani na kukubali kipigo cha mabao 2-0 jijini Madrid lakini ikatinga fainali kwa jumla ya mabao 4-3
.Chanzo:Mwananchi
Mjumbe jr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top