Unknown Unknown Author
Title: MAN U YAICHALAZA ASTON VILLA 4-1
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wayne Rooney akishangilia baada ...
rooney_77d6f.jpg
Wayne Rooney akishangilia baada ya kufunga goli.
Na Riziki Mashaka.
Manchester United imevunja ukimya baada ya kuitandika timu ya Aston Villa magoli 4-1 katika uwanja wake wa Old Trafford, Aston Villa walikuwa wa kwanza kupachika goli kupitia kiungo wake, Ashley Westwooh mnamo dakika ya 13 ya mchezo, wakati timu zote mbili zikifanyiana mashambulizi ya kushtukiza hali ilikuwa ni ngumu kwa upande wa Man United baada ya kuwa nyuma kwa goli 1-0, mashabiki wa timu hiyo walijawa na wasiwasi baada ya kupigwa goli la mapema.
Wayne Rooney alisawazisha goli hilo mnamo dakika ya 20 na kufikia dakika ya 44 Man United walipata goli la pili kupitia mkwaju wa penati uliowekwa wavuni na mshambuliaji huyo (Rooney), mpaka timu hizo zikienda mapumziko mashetani wekundu walikuwa kifua mbele kwa jumla ya magoli 2-1
Manchester United walilishambulia lango la Aston Villa mara mara wakati mtanange huo ulipokuwa ukiendelea katika kipindi cha pili na kufikia dakika ya 57, mhispaniola, Juan Matta alipachika goli na kuiweka kifua mbele timu hiyo kwa jumla ya magoli 3-1, vijana wa moyes walikuwa wakifanya mashambulizi ya hatari katika lango la Aston Villa katika kipindi cha pili.
Javi Hernandez (Chicharito), aliyetokea benchi aliifungia goli Man United mnamo dakika ya 90 na kuiweka kifua mbele timu hiyo kwa jumla ya magoli 4-1, kwa matokeo hayo timu ya Manchester United imefikisha jumla ya pointi 54 na kuendelea kubaki katika nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi hiyo.
moyes_89c07.jpg
Kocha wa timu hiyo (David Moyes) 
Akiongea na skysports Tv, kocha wa timu hiyo (David Moyes) amesema amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na vijana wake na kusisitiza kuwa bado watapigana mpaka hatua ya mwisho ya ligi hiyo.
Mjumbe Jr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top