Unknown Unknown Author
Title: MH370:"PICHA ZAONYESHA MABAKI BAHARINI"
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Picha ya Satelite ikionyesha kinachodhaniwa kuwa mabaki ya MH320 Serikali ya Malaysia imesema kuwa picha mpya za Satelite zimeony...

Picha ya Satelite ikionyesha kinachodhaniwa kuwa mabaki ya MH320
Serikali ya Malaysia imesema kuwa picha mpya za Satelite zimeonyesha zaidi ya vifaa miamoja vinavyodhaniwa kuwa mabaki ya ndege yake iliyotoweka zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Waziri wa usafiri wa nchi hiyo, Hishammuddin Hussein, amesema kuwa picha hizo zilizotolewa na Ufaransa, zinaonyesha vifaa hivyo kuwa zaidi ya mita ishirini kwa urefu.
Hadi kufikia sasa, hakuna taarifa rasmi ya mabaki ya ndege hiyo kuonekana.
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 239, ilikuwa safarini kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Msako uliofanywa baharini na angani, kuitafuta ndege hiyo umeanza tena katika pwani ya Australia baada mawimbi kutulia baharini.
26 Mar 2014

About Author

Advertisement

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top