Unknown Unknown Author
Title: NCHI TATU AFRIKA ZAANZA JUHUDI ZA NISHATI YA NUKLIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ramani inayoonesha nchi tatu barani Afrika zenye juhudi ya kuongeza nishati ya nuklia. Nchi tatu barani Afrika zimeanza juhudi...

Ramani inayoonesha nchi tatu barani Afrika zenye juhudi ya kuongeza nishati ya nuklia
Ramani inayoonesha nchi tatu barani Afrika zenye juhudi ya kuongeza nishati ya nuklia.

Nchi tatu barani Afrika zimeanza juhudi za kuongeza nishati ya nuklia katika mikonga yao ya umeme. Kenya na Nigeria zinataka kuanza nishati ya nuklia wakati Afrika kusini – nchi pekee kusini mwa bara la Afrika ambayo ina mitambo ya nuklia – inataka kupanua uwezo wake. Mpaka sasa, mataifa ya Afrika yamekuwa yakitegemea mifumo ya kizamani kuzalisha umeme – nguvu za maji au mkaa wa mawe. Lakini vyanzo hivyo vimekuwa na madhara ya kijamii na mazingira, na hata kusababisha watu kuhama makazi yao. Lakini swali kubwa linaloulizwa ni jee Afrika ina uwezo wa kuanza nishati ya nuklia?
Kulingana na takwimu za Benki ya Dunia ni chini ya asilimia 10 tu ya jumla ya makazi yote ya watu barani Afrika ambayo yanapata umeme. Hali hiyo kwa namna kubwa inaathiri pia maendeleo ya viwanda na sekta nyinginezo katika bara masikini kuliko yote duniani.
Shida hiyo ya umeme ndio inasababisha baadhi ya nchi za Afrika kutafakari nishati ya nuklia – mfumo ambao unatumiwa katika baadhi ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea kama vile Marekani, India na China.
Kelvin Kemm, mtaalam wa fizikia ya nuklia huko Afrika Kusini, anasema Afrika inahitaji kuangalia nje ya mifumo ya uzalishaji umeme inayotumika sasa. Anasema "kwa jumla inapata umeme unaotokana na nguvu ya maji, na kila mtu anajua kuwa ukame wa miaka kadha barani humo unawezekana. Kwa hiyo ni hatari kujenga uchumi kwa kutegemea umeme unaotokana na maji."

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top