Ripoti iliyosubiriwa kwa hamu
kuhusu ufisadi nchini Afrika Kusini, imemkosoa vikali Rais Jacob Zuma
kwa kujinufaisha na pesa zilizotumiwa kuikarabati nyumba yake binfasi
katika mkoa wa Kwazulu Natal.
Ukarabati huo uligharibu dola milioni 23.Katika ripoti yake , mdhibiti wa mali ya umma nchini humo,Thuli Madonsela, amesema kuwa Zuma alikiuka sheria za maadili na kujifaidisha na pesa za Umma.
Inaarifiwa Zuma alisisitiza ukarabati huo, ufanywe.
Hata hivyo, ripoti hiyo ilisema kuwa hakudanganya wabunge kuhusu kashfa hiyo. Kadhalika wito umetolewa kuwa Zuma arejeshe sehemu ya pesa hizo ambazo hazikutumika kwa ajili ya usalama wake au vinginevyo.
Vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa baadhi ya pesa za umma zilitumiwa katika kufadhili mahitaji ya kifahari ya bwana Zuma kama bwawa la kuogelea na chumba cha sinema.
Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kuwa ripoti hiyo itaathiri pakubwa sifa ya Zuma na chama tawala ANC, huku akijiandaa kwa uchaguzi mkuu katika kipindi cha wiki sita.
Chanzo:BBC
Mjumbe Jr
Post a Comment