Wamachama wa Umoja wa Mawakala wa Pembejeo Mkoani Iringa wakiwa
katika kikao cha kukanusha taarifa ya vyama vya siasa juu ya
kuwashutumu kuchukua shahada za wapiga kura za wananchi Jimbo la Kalenga
Mwenyekiti
wa Muda wa Mawakala wa Pembejeo Mkoani Iringa Enock Ndondole katikati
akiwa na watendaji wake wa Umoja wa Mawakala wa Pembejeo, wakikanusha
taarifa ya vyama vya Siasa kwenye vyombo vya Habari leo.(Picha na Martha
Magessa)
Na martha Magessa-Iringa
Tume ya
umoja wa mawakala mkoani Iringa yakanusa taarifa iliyowahusu mawakara wa
pembejeo za kilimo wilaya ya Iringa kuchukua shahada za kupiga kura za
wananchi wa jimbo la kalenga kama dhamana ya kukopeshwa pembejeo.
Akiongea
na vyombo vya Habari leo Mwenyekiti wa Muda wa mawakala wa pembejeo
mkoani Iringa Enock Ndondole amekanusa taarifa hizo iyo iliyotolewa na
vyama vya siasa katika mkutano wa tume na viongozi wa siasa uliyofanyoka
tarehe 12 machi 2014 mkoani hapo.
Mwenyeki
huyo, kwa niaba ya umoja wa mawakala mkoani Iringa amekanusa taarifa
hiyo kuwa si ya kweli na kusema kuwa jukumu la mawakala hao ni kusambaza
pembejeo kwa malipo taslim na siyo kukopesha kwa mujibu wa sheria za
usambazaji wa pembejeo za Ruzuku na kwa mujibu wa makubaliano na
makampuni ya pembejeo na si vinginevyo.
Aidha
ameiambia jamii kutotafasili vibaya kwa mawakala hao kuwa wamezuia
shahada za wananchi na kuwanyoima haki zao cha kupiga kula.
Hata
hivyo,umoja wa mawakala mkoani Iringa imejulisha Umma na Serikali kuwa
habari hizo si sahihi bali ina lengo la kuwachafua mawakala wa pembejeo
za kilimo.MJUMBE Sr
Post a Comment