Haikuwa na jeraha lolote. Ndugu zake walipopata taarifa za msiba, waliuchukua mwili na kuusitiri harakaharaka.
Hawakuwa na wasiwasi wowote wa kutaka kujua chanzo cha kifo cha ndugu yao kwani waliamini kuwa amefariki dunia kwa sababu ya kuzidiwa na ulevi, kwa kuwa siku zote alikuwa mlevi kupindukia. Kumbe, walikuwa wamekosea, kwani siku hiyo Louis hakuwa amelewa, bali kifo chake kilisababishwa na majambazi waliompora fedha kabla ya kumnyonga hadi kufa.
Yapo matukio mengi ya namna hiyo katika sehemu mbalimbali nchini, lakini mengi kati ya hayo hayafanyiwi uchunguzi wa kujua chanzo.
Daktari wa Kitengo cha Uchunguzi wa Magonjwa na Kiongozi wa Idara ya Uchunguzi wa Vifo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Innocent Mosha anasema ni muhimu kufanya uchunguzi wa sababu za kifo ili kujiondolea shaka au wasiwasi wa kipi kilisababisha kifo hicho.
Dk. Mosha anaelezea maana ya uchunguzi wa kifo na kusema kuwa ni kitendo cha madaktari kutafuta chanzo kilichosababisha kifo cha mtu na kujiridhisha au ndugu kuridhika pasipo shaka.
“Watanzania walio wengi bado hawafahamu umuhimu wa kufanya uchunguzi wa vifo vya ndugu zao, jambo ambalo linasababisha wakati mwingine kupoteza ushahidi au kukosa cheti cha kifo ambacho kina umuhimu mkubwa katika masuala ya mirathi,” anasema Dk Mosha
Anasema uchunguzi wa kifo si kwa ajili ya polisi wa upelelezi tu, bali ni mchakato unaotakiwa kufanywa na ndugu wa marehemu ili kujiridhisha na sababu ya kifo cha ndugu yao.
Anaongeza kuwa tatizo kubwa hapa nchini ni kuwa watu wengi hawaelewi maana na umuhimu wa kuchunguza miili ya ndugu zao ili kujua chanzo au sababu za vifo vyao.
Mchakato wa Uchunguzi
Kwanza, Dk. Mosha anasema uchunguzi wa kifo kwa matukio yanayohusisha polisi, huhitaji taarifa ya utangulizi ambapo polisi hutakiwa kutoa maelezo ya awali kuhusu marehemu.
Anasema pia kuwa katika matukio hayo, ndugu zaidi ya mmoja huhitajika kwa ajili ya kumtambua marehemu, sanjari na kujaza fomu ya maelezo mafupi. “Baada ya polisi kutoa maelezo yao ambayo kwa kawaida huwa ni mafupi, daktari huendelea na uchunguzi wake kulingana na ujuzi wake,” anasema.
Chanzo:Mwananchi
Mjumbe Jr
Post a Comment