Jaji Joseph Warioba.
Baada ya
Wajumbe wa Bunge Maalum kuridhia Kanuni za Bunge hilo na kukamilika kwa
shughuli za kuapa, kazi ya kujadili, kuboresha na kutunga Katiba
itakayopendekezwa ili ipigiwe kura za maoni na wananchi inaanza leo kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba,
kuwasilisha bungeni Rasimu ya Katiba.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samuel Sitta, Jaji Warioba atawasilisha rasimu hiyo kuanzia saa 10 jioni.Sitta alisema Rais Jakaya Kikwete atazungumza na wajumbe wa Bunge hilo Jumanne au Jumatano.
Hata hivyo, alisema wajumbe watapata siku tatu za kujadiliana kuhusu majukumu na mwelekeo wao kuhusu Rasimu ya Katiba mpya.
Kikao cha kwanza cha Bunge la Maalum kilianza Februari 18, mwaka huu, baada ya mkutano wa maelekezo ya ukaaji na jiografia ya ukumbi wa bunge uliofanyika kwa wajumbe, majira ya asubuhi, na baadaye mchana lilisomwa Tangazo la Rais la kuitisha Bunge Maalum, na baadaye walifanya uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti wa muda wa bunge hilo ambapo Pandu Ameir Kificho, aliwashinda wenzake Profesa Costa Mahalu (MJ) na Margareth Rwebangira.
Baada ya hapo wabunge walipata mafunzo ya siku moja kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, yaliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, Februari 19 na siku ya pili yake walianza semina kuhusu Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo, iliyowachukua muda wa siku 21 hadi kukamilika.
Chanzo:Mjengwa(J.G)
MJUMBE sr
Post a Comment