Na Said Ng'amilo
Iringa.
Wanawake na vijana wametakiwa kujiunga katika vikundi vya kiuchumi na
hatimaye kupata mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kuanzisha na
kuendesha biashara kutoka Benki ya Wanawake (TWB).
Akizungumza
na Waandishi wa habari mjini hapa, Mkuu wa Shughuli za utendaji na
maendeleo ya Benki, Yebete Zabron alisema vijana wengi wanapomaliza vyuo
wana mtizamo wa kuajiliwa jambo ambalo limepitwa na wakati kutokana na
ugumu wa kupata ajira zenyewe na mabadiliko ya kiuchumi duniani.
Alisema
jambo la msingi ni kujiunga katika vikundi vidogo vidogo vya kiuchumi,
kupatiwa mafunzo ya jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara na
haatimaye kupata mikopo yenye masharti nafuu.
Alisema
jamii inatakiwa kuachana na mazoea ya kwenda kukopa mitaani kwa riba
kubwa wakati kuna taasisi za kifedha kama benki hiyo ambazo zinatoa
mikopo yenye masharti nafuu na kwa riba ndogo ikilinganishwa na ile
inayotozwa kwenye vikundi vilivyo nje ya mfumo rasmi.
Zabron
alisema lengo la benki hiyo ni kuwainua wanawake kiuchumi kwa sababu
wamekuwa nyuma katika familia licha ya kuwa na umuhimu katika ustawi wa
familia na jamii kwa ujumla.
Alisema
pia kwa hapo baadaye wataanza kutoa mikopo ya bodaboda na bajaji ili
kuwasaidia vijana wengi kuingia kwenye biashara hiyo na kuongeza vipato
vyao.
Alisema
hivi karibuni watafungua huduma ya benki wakala ambapo wataweza kutoa
huduma zote za kibenki kupitia mawakala hao ambao watakuwepo katika kila
wilaya na kila ilipo ofisi ya Posta lengo likiwa kuafikia wenye kipato
cha chini wote.
Hata
hivyo alitahadharisha kuwa ni vema mikopo ambayo wanawake na vijana
watachukua waitumie vyema na si kwa ajili ya kuongeza nyumba ndogo na
kufanya starehe bali ilenge kufanya maendeleo ya familia.
Afisa
mikopo Msimamizi wa Iringa, Baker Gunje alisema mteja wao hafungwi
kurejesha mkopo haraka na kuweza kupata mkopo mwingine na kwa kufanya
hivyo riba yake itapunguana kuwa wanatoa mikopo ya kuanzia Sh200,000
hadi 2,000,000.
Mkuu wa
Shughuli za Kibenki na Maendeleo ya biasharaYebete Zablon akongea na
waandishi wa Habari Mkoani Iringa kuhusu adhima ya TWB kufika mkoani
hapo na kuanza shughuli zake za utoaji mikopo yenye asilimia ndogo kwa
wafanyabiashara wadogo na wajinsia zote wa Iringa.
(Picha na Said Ng'amilo)
(Martha Magessa)
MJUMBE Sr
Post a Comment