Unknown Unknown Author
Title: IMAM MAKABURI AUWAWA MOMBASA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hali ya wasi wasi imetanda huko Mombasa kufuatia kifo cha Sheikh Abubakar Shariff Ahmed, maarufu kwa jina la Makaburi aliyewekewa vikwa...
462ECBA4-1C4E-430D-A271-56569B0C2AA9 w443 r1 17a2d
Hali ya wasi wasi imetanda huko Mombasa kufuatia kifo cha Sheikh Abubakar Shariff Ahmed, maarufu kwa jina la Makaburi aliyewekewa vikwazo na Marekani na Umoja wa mataifa kwa msimamo wake wa kuunga mkono kundi la Al-Shabab, pamoja na kuwaandikisha vijana kujiunga na kundi hilo. makaburi amekuwa akikanusha tuhuma hizo
.
Polisi inaeleza kwamba mauaji hayo yaliofanywa na watu wasiojulikana wenye silaha yametokea baada ya serikali ya Kenya kutangaza kwamba imeanza operesheni ya kuzuia wimbi la mashumbilizi nchini humo, na kwamba maafisa wa polisi wamewakamata zaidi ya watu 650 huko Nairobi kufuatia milipuko mitatu ya bomu mjini Nairobi siku ya Jumatatu.
Ripoti ya kuuliwa kwa Sheikh Abubaker Ahmed -'Makaburi'
Wakili wa Imam Ahmed, Mbugua Murithi amesema Sheikh Ahmed aliuwawa pamoja na mtu mwingine asiyejulikana karibu na jela ya Shimo la Tewa nje ya mji wa Mombasa.
Akizungumza na Sauti ya Amerika Amin Mwidau, mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Toronto Canada, anasema ni kitendo cha kusikitisha lakini anasema mauaji hayo yanatishia kuleta ghasia za kulipiza kisasi.
Mwidau anasema hatari iliyopo kutokana na mauwaji yake kuna uwezekano wa wafuasi wake na watu wengi kuamini zaidi mawaidha yake kwamba waislamu wa Pwani Kenya wanakandamizwa.
Makaburi ni Imam wa tatu kuuliwa Mombasa katika kipindi cha chini ya miezi 6.
chanzo:VOA

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top