Kuna sauti
zimeanza kujitokeza za kuhoji uhalali wa muungano wetu. Hii sio mbaya
kama nia na dhamira ni kurekebisha na kuibuka na muungano imara na
madhubutu zaidi. Lakini tuangalie tusijekujikuta tunafanya kazi ya watu
wengine kwa kujua au kutokujua. Mimi nadhani tunaweza kabisa kudai
serikali tatu bila kukejeli muungano huu. Kwa maoni yangu sioni mantiki
ya kuhoji uhalali wa muungano huu miaka 50 baadaye. Tungependa kuona
pande zote mbili zenye kutaka serikali mbili na tatu zikilenga
kuimarisha muungano huu ili nchi Tanzania iendelee kudumu na kuwa imara
zaidi.
Msingi muhimu wa majadiliano uwe kuhakikisha kwamba hatuvunji nchi tuliyoijenga kwa miaka 50.
Chanzo:Kitila Mkumbo
MJUMBE Sr
Msingi muhimu wa majadiliano uwe kuhakikisha kwamba hatuvunji nchi tuliyoijenga kwa miaka 50.
Chanzo:Kitila Mkumbo
MJUMBE Sr
Post a Comment