Unknown Unknown Author
Title: MAMA GETRUDE MONGELA NA KISA CHA CHAI YA JIONI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
“Unajua enzi zetu hapa chuo ( Mlimani ) kila kitu ilikuwa bure; kula bure..kulala, n.k Mtu unaripoti chuo, unafanya usajili, kisha una...

“Unajua enzi zetu hapa chuo ( Mlimani ) kila kitu ilikuwa bure; kula bure..kulala, n.k Mtu unaripoti chuo, unafanya usajili, kisha unaonyeshwa pa kulala, baasi! Hakuna kulipa ada. Nakumbuka mpaka leo nilipokuwa nalala. Ilikuwa ni Hall 5 ghorofa ya 7!
“Halafu enzi hizo tulikuwa Waingereza kwelikweli, we were very British! (Kicheko). Ukiachilia mbali ratiba ya kawaida ya chakula, kulikuwa na ratiba ya chai ya jioni pia..chai ya saa kumi. Unatoka zako kusoma unapitia kafeteria unapata chai! Mara nyingine, wakati wa mitihani kulikuwa na chai ya usiku pia..’Unapiga kitabu’ maktaba halafu saa nne unakwenda kupata chai!
Sasa turudi kwenye habari ya chai ya jioni. Kulikuwa na utaratibu umejengeka kwamba chai ya jioni ilikuwa ni kwa ajili ya wanaume pekee, ni wanaume pekee walijaa cafeteria wakati wa chai ya jioni! Baada ya muda utaratibu huu ukakomaa na kuwa utamaduni kabisa, wanawake hawaruhusiwi kukanyaga kafeteria wakati wa chai ya jioni. Ni chai ya wanaume! ( Kicheko)
Sasa siku moja muda wa chai ulipowadia, tukajongea kupata chai. Cha kustaajabisha, siku hiyo tukakikuta kikundi cha wanawake pale Kafeteria. Halafu kulikuwa na mwanamke juu ya meza akipaza sauti kwa nguvu…”Mfumo huu ni kandamiziiii!” Chai ya mchanaa ni haki kwa woteeee! Chai ya mchana ni kwa wanaumeee na wanawakeeee! Ubaguzi mwisho leoo! Wenzake walikuwa wanamshangilia kwa nguvu. Hapo tukajua mapinduzi yametokea. Kuanzia siku hiyo, iliyokuwa chai ya wanaume ikawa chai ya wote.
Je munamjua mwanamke aliyesimama juu ya meza? Alikuwa ni Getrude Mongella.
…………………..
Hii ni tafsiri yangu ya simulizi ambayo Profesa Chriss Peter Maina alitusimulia darasani siku moja akikazia jambo fulani.


IME SIMULIWA NA ADO SHAIBU

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top