Unknown Unknown Author
Title: RAIS KIKWETE APONGEZA TIMU YA WATOTO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya watoto wa Tanzania iliyonyakua kombe la dunia Rais wa Tan...

Timu ya watoto wa Tanzania iliyonyakua kombe la dunia
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza Timu ya Watoto wa Mitaani ya nchi hiyo kwa kutwaa Kombe la Dunia huko Rio de Janeiro nchini Brazil.
Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Tanzania imesema Rais Kikwete afurahishwa jinsi watoto hao walivyonyakua kombe hilo la dunia.
"Mmetuwakilisha vyema, ninawapongeza sana, pia mmewapa moyo watoto wengine wote wenye vipaji maalum lakini hawakubahatika kuwa na makazi rasmi, hongereni sana" Rais amesema.
Timu hiyo ya watoto wenye umri chini ya miaka 16 ilipangwa kundi la 2 ambapo pia zilikuwapo timu kutoka Nchi za Argentina, Nicaragua,Philippines na Burundi.
 Chanzo:bbc

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top