
Mboka akiwa na mtoto wake baada ya kukabidhiwa na polisi.
Na Godfrey Kahango, Mwananchi
Posted Jumanne,Aprili29 2014 saa 10:31 AM
Posted Jumanne,Aprili29 2014 saa 10:31 AM
KWA UFUPI
- Mboka na mwanamke huyo waliondoka kwenda kwenye zahanati hiyo kwa pi
Mbeya. Aprili 6, mwaka huu ni siku ambayo mkazi wa Kijiji cha Kibanda wilayani Kyela, Mboka Mwakikagile (20) haitaisahau.
Ni siku ambayo aliibiwa mtoto mchanga wa kiume aliyekuwa na umri wa siku saba tu.
Akisimulia tukio hilo, Mboka anasema alijifungua salama Machi 30 akiwa nyumbani kwa wazazi wake ambao ni Lupalo Mwakikagile (90) na mkewe Nelly Kyusa (49).
Anasema akiwa katika siku ya saba, alipigiwa simu na mzazi mwenzake (jina linahifadhiwa) kwamba mama yake mkubwa atafika nyumbani kumwona mtoto.
Anasema baada muda mfupi mwanamke huyo alifika kwa pikipiki akiwa na mkoba uliokuwa na nguo za mtoto, sabuni na vifaa vingine. “Baada ya kumkaribisha na kusalimiana na wote , mwanamke huyo alimchukua mtoto na baadaye alinishauri twende Zahanati ya Njisi akatibiwe jicho ambalo lilikuwa linamsumbua kidogo,’’anasema.
Mboka na mwanamke huyo waliondoka kwenda kwenye zahanati hiyo kwa pikipiki na kwamba baada ya kufika hapo, daktari aliwataka wanunue daftari na mwanamke huyo alitoa Sh2,000 na kumtaka akanunue.
‘’Nilipokea fedha hizo na kumwachia mtoto pamoja na simu yangu wakati mimi nikielekea kununua daftari kwenye duka lililo mbali na zahanati hiyo,’’ anasema.
Anasema mara baada ya kurudi dukani alishtuka kutomwona mwanamke na mtoto wake.
Anaongeza kuwa alimwomba daktari simu na kumpigia mzazi mwenzake ambaye alimjibu kwamba asiwe na wasiwasi kwani inawezekana alitoka mara moja.
‘’Nilikwenda eneo la bodaboda na kuwauliza madereva kama walimwona mwanamke akiwa na mtoto. Walikiri kumwona akiwa na wasiwasi na kwamba alipanda pikipiki na kuondoa,’’ anasema.
Anasema baada ya kuambiwa hivyo, aliangua kilio jambo lililowafanya majirani wa eneo hilo kutaharuki na kufika kumpa pole.
Mboka anasema alikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Kasumulu , lakini cha ajabu alipofika alimkuta mzazi mwenzake akiwa kituoni hapo.
Chanzo:Mwananchi
Na Mjumbe Jr
Post a Comment