Unknown Unknown Author
Title: SOMO MURUA KWA WALE WANAO TAMANI KUWA WAJASIRIA MALI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MASWALI 10 UNAYOPASWA KUJIULIZA KAMA UNATAKA KUWA MJASIRIAMALI KWELI Watu weengi  hupenda na kufikiria kuwa wajasiriamali au wafanyabi...

MASWALI 10 UNAYOPASWA KUJIULIZA KAMA UNATAKA KUWA MJASIRIAMALI KWELI

Watu weengi  hupenda na kufikiria kuwa wajasiriamali au wafanyabiashara lkn wengi wao hushindwa, na takwimu zinaonyesha 90% ya biashara nyingi hufa baada ya miaka mitano au kushindwa kupata manufaa kama waanzilishi wa biashara hizo walivyotarajia leo nataka ujiulize maswali kumi kama unataka kuwa mjasiriamali au umekuwa mjasiriamali lkn bado hujafanikiwa maswali haya ukiona huyawezi basi hutaweza kuwa mjasiriamali au kukuza biashara yako.

  1. Kwanini unataka kumiliki biashara? au kuwa mjasiriamali? hichi cha kwanza unapaswa kujua umemuona mwenzako anafanya umependa,kazi imekuchosha,maisha magumu au unapenda kutoka moyoni?
  2.  Unashauku kiasi gani ya kumiliki biashara yako au kuwa mjasiriamali?
  3. Je uko tayari kutumia muda wako kujifunza kuhusu biashara au ujasiriamali? kama unataka kuwa mjasiriamali au uko ni mfanyabiashara halafu hauko tayari kujifunza mambo mbali mbali kuhusu biashara hutaweza na utafeli hapa ndipo wafanyabiashara wengi wanafeli.mtu kamuona rafiki yake kafungua botique na yeye anaenda kukopa pesa anafungua botique bila kupata elimu ya kutosha kuhusu biashara.
  4. Je unaogopa kushindwa? (A re you afraid to fail?) ukijiona unaogopa kushindwa ujue huwezi kuwa mjasiriamali maana mjasiriamali ni risk taker na matajiri wote unaowaona duniani wamefeli mara nyiingi ndio wakafanikiwa.
  5. Je unaweza kubadilisha uoga wako wa kushindwa kuwa jasiri ili uendeshe biashara?
  6. Je uko tayari kujifunza kutokana na makosa? hutaweza kufanikiwa ktk biashara kama hutakosea na hutaweza kufanikiwa kama hutajifunza ulipokosea na kurekebisha.
  7. Je uko tayari kujenga team au unapenda kufanya biashara mwenyewe? kama ukijiona huwezi kujenga team basi itakuwa kazi saana kufanikiwa kwenyebiashara kuna msemo unasema.THE RICHEST MAN IN THE WORLD BUILD NETWORK EVERY ONE ELSE LOOK FOR WORK. laiti kama wafanyabiashara au wajasiriamali woote mngejua jinsi ya kutengeneza network biashara zenu zisingekuwa na msimu miaka yote zingekuwa.ila usijari kama hujui nitafute takufundisha.
  8. Je uko tayari kulipa gharama? watu wengi hutaka kuwa wajasiriamali na wengine huanzisha biashara na kufeli kwa kuwa hawako tayari kulipia gharama za mafanikio yao lazima ulipe gharama na gharama pekee ni kuwasaidia watu wengine wafanikiwe kama unataka kuwa mjasiriamali jiandae kuwasaidia watu wengine weengi wafanikiwe nawe utafanikiwa toa huduma kwa watu wengi.
  9. Uko tayari kuwekeza muda wako leo ili ulipwe baadae? watanzania wengi wanaamini ukianzabiashara leo basi wiki ijayo utakuwa tajiri acha mawazo finyu hakuna mafanikio ya harakaharaka mafanikio yote unayoyaona yanachukuwa muda,na biashara inakuwa kama mtoto huwezi kuzaa mtoto kabla ya miezi tisa.kama hauko tayari kuwekeza muda wako leo ili upate mafanikio baadae usifanye biashara.
  10. Uko tayari kujitoa na kupambana kuhakikisha biashara yako inakuwa? watu wenngi hupenda kuanzisha biashara lkn wao hawako tayali kujitoa kwaajili ya biashara zao yaani unafanyabishara lkn hadi mtu mwingine akusukume hutafanikiwa. 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top