Unknown Unknown Author
Title: TAARIFA KWA UMMA:TMBEYA CITY WATOLEA MAELEZO YA KUHONGWA NA AZAM FC
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TAARIFA KWA UMMA UPOTOSHAJI UNAOTOLEWA DHIDI YA TIMU YETU KUELEKEA MCHEZO WA TAREHE 13/4/2014 Kwanza nachukua n...
20140330_160206_095b1.jpg
TAARIFA KWA UMMA
UPOTOSHAJI UNAOTOLEWA DHIDI YA TIMU YETU KUELEKEA MCHEZO WA TAREHE 13/4/2014
Kwanza nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo wa mpira wa miguu na wapenzi wa Mbeya City Fc popote pale walipo kwa kuiunga mkono timu yao muda wote wa michezo ya ligi kuu inayoelekea ukingoni hivi sasa.Klabu inathamini nafasi ya wapenzi na washabiki katika kujenga timu imara na yenye ushindani kama walivyofanya kwa timu yetu.
Timu yetu ilianza ligi msimu huu 2013/2014 ikiwa na malengo ya kuchukua ubingwa au kuwa katika nafasi za juu za ligi yetu.Hiyo ndiyo dhamila iliyokuwepo kwa viongozi,wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Michezo miwili imesalia kwa timu yetu kabla ligi kuu ya Vodacom kumalizika katika msimu huu 2013/2014.katika safari yetu ya ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu, changamoto nyingi za kiutawala na za kimtazamo kutoka kwa wadau wote wanaohusika na mchezo wa mpira wa miguu nchini tumezishuhudia .Changamoto hizo ni ikiwemo upangaji wa ratiba usiyokuwa na uwiano mzuri,baadhi ya mechi kuamuliwa vibaya na waamuzi wa mchezo,wizi wa mapato ya milangoni unaotokana na mfumo mbaya wa uuzaji wa tiketi,uadilifu mdogo kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana ya kusimamia mpira katika ngazi zote n,k.
Kuelekea mchezo wetu wa tarehe 13/04/2014 dhidi ya AZAM FC kumezuka propaganda chafu na ambazo si sahihi katika ukuzaji wa mpira hasa wa ligi ndogo kama ya Tanzania. Nachukua nafasi hii kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo ambayo yamekuwa sehemu ya propaganda hizo:
1.    Klabu imehaidiwa kununuliwa basi na hivyo inajiandaa kutoa ushindi kwa kwa timu ya AZAM Fc na kuwarahisishia mazingira ya Ubingwa.
Halmashauri ya jiji la Mbeya limekuwa katika mchakato wa kutafuta na kununua basi kwa ajili ya matumizi mbalimbali  ya Halmashauri ikiwemo kutumiwa na timu zake ( Netiboli na Mpira wa miguu)ambazo zote zipo ligi kuu ya michezo husika kwa kufuata sheria ya manunuzi ya Umma. Mchakato huo ulianza  halmashauriilipotangaza  nia hiyo katika gazeti la “the guardian” la tarehe hiyo kwa tender tarehe 8/8/2013o.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01   hii ni baada ya Halmashauri kutenga bajeti ya fedha za makusanyo yake ya ndani  kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na 2013/2014 ili kukidhi haja hiyo.
Tangazo hilo halikupata mzabuni mwenye sifa za kufanya usambazaji wa basi hilo hivyo tangazo hilo lilirudiwa tena tarehe 12/2/2014 katika gazeti la majira kwa Tender No.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 (Re-advitised), Mchakato na maandalizi ya ufunguaji  wa ufanyaji wa tathmini wa zabuni hiyo unaendelea kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma.
Pamoja na mchakato huo hapo juu,pia klabu inaendelea na mazungumzo na wadau mbalimbali wenye nia ya kuwekeza kwa udhamini wa bidhaa zao,moja ya maeneo ya udhamini ni pamoja na ununuzi wa basi la wachezaji  taratibu na makubaliano haya yatakapo kamili umma wa wapenda mchezo wa mpira wa mguu utajulishwa.
Hivyo propaganda hiyo kuwa klabu imehongwa basi si za kweli na si sahii ila zina nia ya kuidhalilisha timu yetu. 
Awadh Ibrahim
 
MJUMBE sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top