Unknown Unknown Author
Title: UPDATES YA BAADHI YA MAMBO YALIYO JILI KATIKA MIKUTANO YA UKAWA,ZANZIBAR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Likes GivenUpdates Mkutano wa UKAWA Kibandamaiti Ule mkutano wa Umoja wa katiba ya wa...

Likes GivenUpdates Mkutano wa UKAWA Kibandamaiti Ule mkutano wa Umoja wa katiba ya wananchi unatarijia kufanyika leo kwa upande wa zanznibar. Mkutano huo u

Sikiliza online hapa FreeZanzibarlive on USTREAM: Political events. Politics




Awali mchugaji Msigwa na Lissu wakiwa kwenye boat kuelekea Zanzibar


Quote By Gwalihenzi View Post
ilivyosasa kibanda maiti

>>UPDATES>>>>

>>kwa sasa nyimbo zinaendela kutumbuiza halaiki
>>wenyeviti wa vyama vya UKAWA, MBATIA, MBOWE , LIPUMBA wameshawasili na wanasalimia wananchi
>>Mtikila naye anapanda jukwaani na kusalimia wananchi

>> Jusa, Seif na mzee moyo na timu yote ya ukawa nao wapo

>>Jusa : Anawashukuru wote waliokuwa ndani ya bunge la katiba na kuendeleza umoja huo.
:Wazanzibari wakiwa ndani ya baraza la wawakilishi wote wanaitetea zanzibar lakini ndani ya bunge la katiba wengine wameufyata kinachowasumbua ni matumbo yao.
>>>>Matangazo online stream yametoweka

HALI HALISI YA MKUTANO KWA SASA

Quote By Tumaini Makene View Post
Quote By Kifai View Post
Watu ni wengi sanaaaaaaa
Quote By RICH OIL SHEIKH View Post
Ismail Jussa anaonea sasa. anasema wanapokuwa kwenye baraza la waw kilishi wote bila kujali vyama wanatetea uzanzibari, lakini kufika dodoma wenzetu wameufyata. anasema alimuuliza mwenyekiti wa bunge siri ya wajumbe kutoka znz kuufyata wakifika dodoma. Jusa anasema kinachowaangaisha/kinachowasumbua ni matumbo yao na maslahi yao binafsi ndo mana wanaufyata wakifika dodoma. inaendelea...
Quote By Tumaini Makene View Post

Hadi sasa watu wameshonana uwanjani kutoa sapoti yao kubwa kwa UKAWA katika kupigania Katiba inayotokana na maoni ya wananchi.

Ameshasimama Prof. Abdul Sheriff kutokea kundi la 201 ambaye amesema wazi kuwa wahuni wa kuhujumu hawatafanikiwa mbele ya UKAWA.

Katibu wa Shura ya Maimamu na Taasisi za Kiislamu amesema taasisi zote za Kiislamu zinaunga mkono Shirikisho la Serikali Tatu na kwamba walitoa maoni yao mbele ya tume na wanaungana na UKAWA kulidai hilo. Hakuna atakayeweza kuhimili vishindo vya UKAWA na wapenda haki na matumaini kwa ajili ya amani ya kweli nchini kwetu, Tanzania.

Ameishambulia Serikali na CCM kwa uchochezi wa kidini, kuwachonganisha Watanzania, kutokana na kauli ya uchochezi iliyotolewa na Waziri wa Serikali ya CCM, aitwae William Lukuvi tena kanisani akiwasema waislamu. Amehoji je mashehe nao wakifanya hivyo, nchi itatawalika?

Ametoa rai kwa viongozi wa UKAWA kuimarisha UKAWA na kuhakikisha kuwa UKAWA haufi.


mambo yanazidi kunoga

Quote By Tumaini Makene View Post
Jussa alipanda kuwakilisha wabunge wote wa UKAWA kutokea Zanzibar. Amewaambia Wazanzibar wawe tayari kuwasaliti na kuwazomea wale wote wanafiki wanaowasaliti wanapofika Dodoma kama Asha Bakari.

Amesema Wazanzibar wawashukuru watu kama akina Freeman Mbowe, James Mbatia, Tundu Lissu, John Mnyika na UKAWA nzima kwa kuwa wamesimama kidete kuitetea Zanzibar tofauti na Wazanzibar wengine kama akina Asha Bakari, Balozi Seif Idd na wawakilishi wote wa CCM kutoka Zanzibar.

Amemtangaza Balozi Seif Idd kuwa adui namba moja wa Zanzibar kwa ububu wake bungeni kama kiongozi mkuu kutoka Zanzibar ndani ya Bunge Maalum la Katiba.

Akaongeza kusema ujanja ujanja wanaotaka kufanya wa kubadilisha sheria ya mabadiliko ya katiba kuondoa sharti la 2/3 anasema wafanye wafanyavyo lakini hawataweza kwa kuwa mtarimbo umeganda.

Jussa akasema yeye alikuwa anaweza uwanja sawa tu lakini mchezaji hasa ni anayekuja punde ambaye ni Tundu Lisu.

Lisu;
Quote By Tumaini Makene View Post
Jussa alipanda kuwakilisha wabunge wote wa UKAWA kutokea Zanzibar. Amewaambia Wazanzibar wawe tayari kuwasaliti na kuwazomea wale wote wanafiki wanaowasaliti wanapofika Dodoma kama Asha Bakari.

Amesema Wazanzibar wawashukuru watu kama akina Freeman Mbowe, James Mbatia, Tundu Lissu, John Mnyika na UKAWA nzima kwa kuwa wamesimama kidete kuitetea Zanzibar tofauti na Wazanzibar wengine kama akina Asha Bakari, Balozi Seif Idd na wawakilishi wote wa CCM kutoka Zanzibar.

Amemtangaza Balozi Seif Idd kuwa adui namba moja wa Zanzibar kwa ububu wake bungeni kama kiongozi mkuu kutoka Zanzibar ndani ya Bunge Maalum la Katiba.

Akaongeza kusema ujanja ujanja wanaotaka kufanya wa kubadilisha sheria ya mabadiliko ya katiba kuondoa sharti la 2/3 anasema wafanye wafanyavyo lakini hawataweza kwa kuwa mtarimbo umeganda.

Jussa akasema yeye alikuwa anaweza uwanja sawa tu lakini mchezaji hasa ni anayekuja punde ambaye ni Tundu Lisu.

Lisu;
Quote By Tumaini Makene View Post
Wazanzibar wanamwita Lissu Christiano Ronaldo. Wananchi wameshangilia balaa alipoanza kwa kuwasalimia kwa jina la Zanzibar Huru na Tanganyika Huru na Shirikisho lenye hadhi kuu ya nchi.

Kwa miaka 50, anasema Tundu Lisu, Zanzibar imekuwa koloni la Tanganyika, Zanzibar imefungwa minyororo na Tanganyika na sio huru tena.

Kwa miaka 50 masuala yote ya nje yamekuwa yakiamriwa Dar es Salaam, Mambo ya Ulinzi yanaamriwa na Dar, masuala ya fedha ya Zanzibar yamekuwa yakifanywa na Dar na kwa hiyo ni koloni la Tanganyika.

Anasema mtia minyororo kwa mtu mwingine naye pia hawezi kuwa huru. Akatolea mfano wa mfunga minyororo wa magereza kuwa naye hawezi kuondoka., hivyo Tanganyika iliyoifunga Minyororo Zanzibar nayo haiko huru.

Akasema Tanganyika ilikana jina lake na kuliondoa kwenye katiba ili iendelee kuinyonya Zanzibar, anasema ilikuwa na Tanganyika huru ni kuwa na Zanzibar huru.

Anamkaribisha sasa Maalim Seif;
Quote By Tumaini Makene View Post
Maalim Seif jukwaani sasa; kaanza kwa kumtambulisha Mzee Moyo ambaye alikuwa Waziri wa Katiba wa Mzee Abeid Amani Karume, Mzee Moyo kasema 'ni tatu, tatu, tatu bila mzaha'. Kasema leo anaacha majembe yazungumze.

Maalim amesema kama wanaogopa Shirikisho la Serikali Tatu, basi yeye yuko tayari kuunga mkono serikali mbili kwa maana ya Zanzibar huru na Tanganyika huru, tofauti na hapo kila mtu na lwake.

Maalim anawatambulisha viongozi wa UKAWA nje ya bunge, akianza na Mosena Nyambabe- Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi.

Maalim Seif akaongeza kusema kuwa kama Kikwete anao uwezo wa kuwadhibiti Wazanzibar basi aende na cha moto kitaonekana.

Amesema kuwa kuna magari yameletwa kwenye mkutano na vikosi vya KMKM, akaasa kuwa ole wake aguswe mtu akasema anazungumza kama Makamu wa Rais, watajua jini liliko Zanzibar, uwanja ukalipuka kwa shangwe na nderemo.

Akapanda Emmanuel Makaidi mzee wa 'Moto moto motoooo...uwachome CCM'...

Quote By Tumaini Makene View Post
Dkt. Slaa amesema kuwa Jeshi la Tanzania halijakosa uzalendo kama walio nao mafisadi wa CCM na serikali yake. Kutokana na uzalendo ambalo JWTZ linao kwa wananchi na nchi, haliwezi kupindua serikali eti tu kwa sababu ni Shirikisho la Serikali Tatu.

Anasema kuwa wanajeshi wetu wamekuwa wazalendo kiasi cha kuvumilia kukosa mishahara, maslahi yao madogo na shida nyingine iweje wafanye hivyo kwa serikali tatu, amesema Kikwete halijui jeshi ndiyo maana amepotoka...

Maalimu Seif aliendelea ambapo aliwasihi viongozi wa UKAWA kujiimarisha na kuulinda UKAWA kwani wabaya wao wanajipanga.

Akasema kuwa wakati wa kutishana tishana umeshapita. Kuendelea kutisha Wazanzibar ni kuwaongezea ari na hamasa.
Quote By Tumaini Makene View Post
Makaidi amesema kuwa Watanganyika wamebakia bila serikali kwa sababu Mwalimu Nyerere Baba wa Taifa aliitupa serikali yote ya Tanganyika kwenye Muungano na Karume hakuitupa yote na ndiyo maana wamekuwa ngaringari leo.

Amewaomba Wazanzibar kuungana na Watanganyika kudai serikali zao...

Makaidi anasema CCM hakuna wanasiasa bali wajasiriamali na ndiyo maana hawataki kujisahihisha kama Mwalimu alivyotaka. Kisha akapanda Mtikila...



Quote By Tumaini Makene View Post
Mtikila; Kinachowasumbua CCM kuhusu serikali tatu ni unywani. Watanganyika wanapumbazwa kuwa uhuru ni mizinga uwanja wa taifa. Anasema kuwa kuwatisha wananchi na majeshi ni ugonjwa wa apedomia. Wanasahau kuwa wanajeshi wana ndugu zao wengi uraiani. Akamalizia kwa kusema saa ya ukombozi ni sasa...
Quote By Tumaini Makene View Post
Mbatia; muungano haukuridhiwa kwa sheria za Zanzibar kwa hiyo ni batili. Anasema Zanzibar kujitangazia mamlaka yake ni kuikomboa Tanganyika. Amesema kuwa wajumbe wa UKAWA kutoka Zanzibar wamewanyima turufu majiCCM huko BMK hivyo asitokee mtu wa kuisaliti Zanzibar.

Amesema kuwa chokochoko za udini zinapandikizwa na CCM, lakini hazitafua dafu. Anasema huwezi kuwa muislamu safi halafu ukahubiri udini na ubaguzi wa aina yoyote, huwezi kuwa Muislam safi kisha ukahubiri matusi na kejeli. Vivyo hivyo kwa mkristo safi.


Quote By Tumaini Makene View Post
Mbowe; maandamano nchi nzima ya kudai Katiba Mpya na bora inayotokana na maoni ya wananchi yanakuja baada ya mikutano ya Zanzibar. UKAWA haitarudi bungeni kushiriki dhambi ya kupingana na maoni ya wananchi, dhambi ya kuhubiri matusi kwa wananchi.

Amesema kuwa UKAWA huu si kwa ajili ya Katiba tu bali ni kwa ajili ya maslahi halisi ya wananchi. Ametangaza rasmi kuvunja Baraza Kivuli na sasa ataliunda upya kwa ushirika na NCCR, CUF CHADEMA.

Wananchi wamelipuka kwa furaha baada ya Kamanda Mbowe kutangaza kuwa UKAWA utaendelea hadi uchaguzi.;
Quote By Tumaini Makene View Post

Prof. Lipumba; wanaopinga serikali tatu kwa kigezo cha gharama hawajielewi. Anasema nchi inaingizwa kuzimu kwa matumizi ya hovyo na mabovu ya serikali kila siku.

Amesema ofisi ya rais inaongoza kwa matumizi ya hovyo. Anatoa mfano ambavyo imekuwa ikitumia mabilioni kwa Rais Kikwete kujitangaza Vasco Da Gama kwa kuzurura ughaibuni.

 Imenakiriwa Jamii Forum

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top