Unknown Unknown Author
Title: UTURUKI KUSHIRIKI MIRADI YA UJENZI NCHINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
...


uturuki_2_6da79.jpg
KAMPUNI tatu kutoka Uturuki zimeingia nchini kwa lengo la kushiriki katika ujenzi kwenye miradi tofauti katika maeneo mbalimbali.Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA ya Uturuki, Orhan Babaoglu, alisema kukua kwa sekta ya ujenzi nchini ndicho kigezo kilichowafanya wafungue ofisi zao.
Akizungumza kwa niaba ya Kampuni ya Bosandra Professional Co. Ltd , Babaoglu alimpongeza Waziri wa Ujenzi, John Magufuli kwa kusimamia sekta hiyo hadi kampuni kutoka Uturuki kufungua ofisi zao nchini. 
"Tumekuwa tukifuatilia uendeshwaji na ukuaji wa sekta ya ujenzi katika mataifa mbalimbali barani Afrika na tumejiridhisha kuwa Tanzania ni nchi inayofanya vizuri katika upande huo," alisema Babaoglu.
Mwakilishi mwingine wa Kampuni ya CEYTUN, Kursat Durak, alisema utendaji wa kampuni kutoka Uturuki unafahamika duniani kote, hivyo ujio wao una lengo la kuamsha ushindani wa ubora lakini pia kuona gharama za utekelezaji wa miradi hiyo zinadhibitiwa kwa kuwa na washindani kutoka maeneo tofauti.
Chanzo:Mjengwa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top