Unknown Unknown Author
Title: WAZANZIBAR MNAJUA KUNA UWEZEKANO MKUBWA KUA TANZANIA SI NCHI HALALI KISHERIA?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
/ Uhalali wa Tanzania kama Taifa bila hati ukoje? Ili taifa lolote liwepo kihalali kwa kisheri taifa hilo lazima lijitambulishe Umoja wa...
/

Uhalali wa Tanzania kama Taifa bila hati ukoje?

Ili taifa lolote liwepo kihalali kwa kisheri taifa hilo lazima lijitambulishe Umoja wa Mataifa UN na umoja huo ulipitishe rasmi usiibitishe rasmi kwa taratibu za kisheria, sasa iulizwe Umoja wa Mataifa nakala hizo zipo ? Na allegation ya Wazanzibar ilikua ni nani na nani walo iwakilisha Zanzibar kipindi hicho?.

Na jee hii Tanzania nayo pia ilipitishwa rasmi kule UN kama Taifa huru,United Republic of Tanzania ? Tusikubali kuambiwa Mtanganyika katuwakilisha itakuwa ni kama Wazanzibar ni disable?.

Tufike pahali sasa tujiulize hivi kweli Taifa hili la Tanzania lipo kisheria kwa mujibu wa Ummoja wa Mataifa?.
Andamana na mimi katika ziara hii fupi kukufanyia uchaambuzi wa uhalali wa Taifa la Tanzania.
ikiwa Ummoja wa Mataifa UN yaikana SMT hadharani kuwa wao hawana hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ? Sasa munataka usibitishoo (proof) kutoka wapi tena Wazanzibar?.

Muungano kama huu wa Mdomo ni Muungano wa Ajabu sana uliosalia Dunia hii , kwani Muungano huu licha ya kudumu kwa miaka 50 , lakini hauna uhalali tayari una mushkeli kisheria kwa hio Wazanzibar tuwe makini na maneno ya mkato ya Watanganyika akina Sumuel Sitta na Ndugu zake kua Umeishi miaka 50 na Mkke wako halafu unauliza cheti cha ndoa kiko wapi?.

Haya ni Maneno ya kutuzuga tu ,kuzani rabda Wazanzibar ni pofu, tuwe na tahazari sana na ulahai na ujanja huu kwa jambo kubwa kama hili la kisheria ,kifupi kama hatuja hakikisha Mkataba halali wa Muungano tuishie hapo tukenda mbele zaidi kiza na tutakumbana na mambo mengi yatakayo tuzonga.

Ukweli ni kuwa Mkataba wa Muungano, “Articles of Union”ni mkataba uko kisheria zaidi unavipengele vya kisheria na unatawaliwa na sheria na unajulikana Sheria na Kimataifa (international law) na vile vile unakufunga kisheria kwa mujibu wa sheria.

Sasa hayo ya Mh Samuel Sitta ni Upuzi mtupu usio na mashiko hayo unaweza kuzungumza katika halmashaurii kuu yenu ya ccm ,sio Kwa Wananchi wa Zanzibar kutaka kujua ukweli wenyewe .

Inawezekana ni sisi wenyewe Wazanzibar tumejipweteka hatujenda deep, lakini hata hio Tanzania iloko UN kwa vile Hati ya Mkataba haiko UN inawezekana hivyo uanachama wenu UN could be a lie!. We are existing a lie, living a lie and continue lying!.

Wazanzibar tukikubali kuendelea nao Muungano huu wa ajabu?, Basi tutaonekana na sisi ni watu wa majabu vile vile,Maana hata Sherehe za Tanganyika independence ,utasikia Sherehe za Tanzania Bara?.

Hii ni kutaka kuficha ukweli halisi wakua Washalikoroga na sasa wanababaisha mambo ili watu wajichanganye. Wazanzibar tuwe macho ?.

Liko kundi dogo hapa Zanzibar linafaidika na mazingaombwe haya na mazingira haya kwa kupewa pesa za budget kiulaini kwa kisingizio cha kumaliza kero za Muungano, kero hizo za Muungano hazipo Maana huo Muungano haupo na wala haujawahi kuwepo upo Usaaanii tu wa ccm.

Watu hao (All they know is lies nothing else).ili Mradi waoo wa Utapeli uendelee kuwa-foolish Wananchi na Kumauni pesa kwa kuchungulia Wazanzibar bado hawaja amkaa?.

Kwa mantiki hii hatuna haja kupoteza muda na pesa za Umma kujadili katiba ya muundo wa Serikali kwenye Muungano wakati Muungano haupo,Wala haujawahi kuwepo.

Labda kabla hatujandika katiba mpya, turekebishe makosa, lets make things right kwa Tanzania kuwa na Mkataba halali kabisa wa Muungano ambao njia pekee ya kuupata ni kupitia referandum kwa Wananchi .

Tuanze sasa kujadili kuungana kwa kufuataa utaratibu wa kisheria.Wala hakuna haja kuhofu kuwa Muungano utavunjika kwa sababu Muungano haujawahi kuwepo ni ujanja tu ulotumika na ubabaishaji .

Ni Muungano gani huu Duniani ulokua hauna hati za kisheria wananchi wa pande mbili za Muungano Dunian wanao weza kukubalii kama sikufanyana Majuha? Tukubali hakukua na Muungano ili tuanze mambo from basement?.

Tena wahusika wote wa Nyerere watuombe radhi wananchi kwa ulahai huu na utapeli huu waliotufanyia kabla hatuja waburuza katika mahkama za kimataifaa na sheria kuchukua mkondo wake.

Ndio tukambiwa na hao Wajanja wa Nyerere ,kua Muungano tusiunguse,tusiujadili wala tusiuhaji , Bali tulinde ,tuenzi na tudumishee? Sasa haya yote ni kujua fika Nyerere kua Muungano siwoo, na alitumia ujanja na vitisho ili kuziba mazambi yake alokwisha fanya.

Tutayajua mengi mwaka huu. Kweli hakuna uongo wa kudumu ila uko ukweli wa kudumu hata uufiche vipi.

Watu wengi wanatushaangaa Wazanzibar ,huu ni Muungano gani usokua na Hati za Mkataba?, na vile vile tujitazame Muungano huu ni kama vile wa Sisimizi na Tembo hauingii akilini kabisa.

Nyerere alijifanya mjanja lakini Mh Karume na Wajumbe wa Memba Baraza la Mapinduzi walikua wajanja zaidi,Si kwamba kuku akinya chooni sio kama ana akili bali alienda kutafuta chakula tu.

Tufika pahali Wazanzibar tuseme kama hakuna Hati ya mkataba halali basi huwezi kuleta mpango wa kienyeji anyeji ,huu ni Muungano wa Dola mbili huru na watu wake, tusikubali kuletewa ujanja na ulaha.

Ingekua Watanganyika ni wao tulio watawala na kuwafanyia hivi basi mawakili ilekua wanapishana kwenye Mahkama za kimataifaa .

Semeni ukweli kua Hati ya Muungano haipo sio kubabaisha , kwa vigezo vya umedumu kwa miaka 50 eboo, udumu miaka 100 lakini ikiwa kulikua na Udanganyifu basi hakukua na nia safi ya jambo hili .

Tunataka tuwaulize wale wote vizabi zabina akina Shamsi Nahodha na Yahya Hamadi walosema hati ipoo ipoo? Ipoo wapi UN na Makkama kuu , Walishwe Yamini wameiona ? Au ndio walikubali kulishwa maneno ya uongo ili kuliteketeza taifa la Zanzibar na kizazi chake ?.

Hivi sasa tunachokidai Wazanzibar ni mkataba halali original Document na sio Kero za Muungano kutatuliwa na Katiba ijayo ,sisi tukomalie hapo hapo kwenye mkataba, ikiwa Mkataba halali hakuna hizo kero za Muungano zitakua na mashiko gani kutatuliwa kwenye katiba?

Ikiwa hakuna Hati ya Mkataba UN basi hakuna Muungano kuna ushirika na urafiki wa kivyama tu ,lakini kwa Mujibu wa Sheria Muungano utakua ni (illegal) .

Nakama Wananchi wa Zanzibar hatukujifunga kutaka kufuatilia Uhalali wa Muungano huu kimataifaa na kuonyeshwa Hati ya Mkataba iloko UN, basi katiba hii itakua haina maana hata wa irembe vipi si kwa Serekali tatu au kuku Bali mkataba .

Kwanza kabla ya Kujadili rasimu ya Katiba nilazima tujuwe ukweli hasa wa jambo hili ,sio leo kesho tukaja kugeuziwa kibao kua mfumo wa Serekali tatu umekubalika na sasa Tanganyika imevua Koti la Muungano no.

Tujue uharamia huu kwanza , hayo mengine yote yatapatiwa ufumbuzi bada ya kujua uhalali wa Muungano kwanza ukoje?.

Bila ya kuto kujikaza wananchi wa Zanzibar ,tuneless kufanyiwa vilinge huko mbeleni kwa kumiminwa Watanganyika na itakuwa yale ya Palestina kulengea mawe.

Tusikubali Wazanzibar kulainishwa kwa kuambiwa Muungano sasa umedumu kwa miaka 50 na sisi ni ndugu wa damu, hizo ni hoja zaifu ,tujue kwanza uhalali wa Muungano bila ulahai vitisho au ubabaishaji.

Historia za nchi zote ambazo zilikuwa au zenye miungano ya ku force huwa zinaishia kutengana, hivyo hata kwa Muungano huu wa Ku-foce utavunjika tu kwa vile hakuna ridhaa ya wananchi.

Imekuwa kama zile ndoa ambazo kila leo mke anakung’utwa na mumewe na anasema ati anabakia kwa ajili ya watoto tu!

Kama kusema ni undugu kwa nini hawakuungana na Kenya mbako makabila yanaingiliana kiudugu na Tanzania , ambako kote kuna Wajaluo na Wamasai? Au Malawi na Msumbiji kwa Wamanda na Wamakonde yote ni makabila hayo Wanayo Tanzania na nchi zao ni boarder za mipaka ?

Wabara wengi wanajifanya kusahau kujua kua Zanzibar ilikua ni Dola huru na sio mkoa au Wilaya na ,wengi wa Wazanzibar hawaupendi Muungano huu si kwa siasa za ccm kuwabagua tu ,bali hata kwa ridhaa umefeli kuwa Muungano.

Katika maktaba za Ummoja wa Mataifa UN hakuna Mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa.

Waulizeni Nduguzetu waloko kule watawambia ,na kwanini iwe hivyo? Nchi zote ukenda kwenye Maktaba za UN utaona iko wazi ukingia kwenye kumbukumbu zao why sisi uwe siri?.

Chanzo:Zanzibar news
Mjumbe Jr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top