>>VIINGILIO 5,000/=, TIKETI KUUZWA KUANZIA SAA 2 ASUBUHI JUMAPILI!
WAKIWA chini ya Kocha Kocha mpya , Mart
Nooij, kutoka Holland, Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, watacheza
Mechi yao ya kwanza ya Kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Malawi,
Flames, Jumapili kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mjini Mbeya.
SOMA ZAIDI:
Release No. 075
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 2, 2014
MALAWI YAWASILI, KIINGILIO 5,000/
Timu
ya Taifa ya Malawi (Flames) imewasili jijini Mbeya tayari kwa mechi ya
kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Mei 4 mwaka huu)
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Flames ikiwa na msafara wa watu 31
imewasili jana (Mei 1 mwaka huu) saa 1 jioni kwa njia ya barabara, na
imefikia hoteli ya Manyanya. Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager ipo jijini Mbeya tangu Aprili 27 mwaka huu
kujiandaa kwa mechi hiyo.
Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa sh.
5,000 wakati tiketi zitauzwa siku ya mchezo kuanzia saa 2 asubuhi
katika vituo vya Uyole, Mwanjelwa,, Mbalizi, Stendi Kuu, Holiday Inn na
Uwanja wa Sokoine.
Magari yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani ni ya wachezaji, gari la wagonjwa, gari la zimamoto na gari la waamuzi pekee.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
MJUMBE Sr
Post a Comment