Unknown Unknown Author
Title: MASAA MATANO YA SUMBAWANGA HADI:MBEYA "MWANANGU VIJANA MNAO IPINGA CCM HAMUJUI ILIKO TUTOA!"
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
 Leo Asubuhi Natokea Mtaa wa Majengo,Sumbawanga Kuelekea Stendi Wadau Leo Asubuhi Nime Anzia Safari yangu pale Stendi kuu ya Rukwa/Sumba...
 Leo Asubuhi Natokea Mtaa wa Majengo,Sumbawanga Kuelekea Stendi

Wadau Leo Asubuhi Nime Anzia Safari yangu pale Stendi kuu ya Rukwa/Sumbawanga! Nime Jitahidi kuukatiza Usingizi wa Asubuhi ili tu Niwahi Usafiri....! Jamaa yangu akawa ananitania kuwa
 "Huku Madereva wanazingatia sana Muda wa Kuondoka... Usije ukadhani ni sawa na Wale wa Stendi ya Mbeya..."

 Nikilipia nauli ya Sumbawanga Mbeya Stendi,Dakika Mbili Tiari kwa Kuanza Safari kuanza

Kuna Msemo Maarufu kuwa Usije Uka yasifu Mapishi ya Mama yako Wakati hata Hauja wahi Toka nje ya kijiji Chako Ukala Chakula huko"

Nimepewa Kiti ambacho nilizungukwa na Weneji wa Rukwa haswaa,Nika Kaa katikati yao ili nimalizie Ule usingizi wangu nilio ukatiza! Nasalimia;Huku nikiegemea Kiti kwa Uchovu...Haikuchukua hata nusu saa kabla Mazungumzo kati yangu na Majirani wangu  hayaja anza,Huku kila mmoja akijaribu kutoa maoni yake ya jinsi anavyo ijua Rukwa/Sumbawanga.
Huku nikiwa nawasikiliza 'Sumbawanga inakua kwa kasi sana kiasi kwamba kama kuna mtu alikuja miaka Mitano iliyo pita anaweza akashangaa jinsi mkoa huu unavyo kua'.


 Uelekeo wa Niliko tokea(Rukwa);Nime Mwomba Dereva Tuchimbe Dawa(Kumbe nina Taka Nichukue Taswira ya Barabara ya Sumbawanga Mbeya

   Ninako Elekea Mbeya na hapa Nime Shuka Kuchimba Dawa(Na Kamera yangu hivi ndio nachimba Dawa)

Mwingine Ukiwa unaishi mbali na Sumbawanga picha inayo kujia kwa haraka ni Uduni wa Maisha na ugumu wa kufikika kwani enzi Zetu ilikuwa una weza kutoka Mbeya Asubuhi na Ukafika Sumbawanga Saa tatu Usiku wakati Leo Asubuhi ya Saa Tano Tuta kuwa Tumesha Fika Mbeya!
Mzee aliye amini nina Msikiliza na ninatamani nimpinge anacho kiongea huku akinikazia macho Unajua mwanangu vijana Mnao ipinga CCM Hamujui iliko tutoa,Mme kuja Kipindi ambacho kila kitu ambacho kilikuwa kero enzi zetu kimesha patiwa ufumbuzi ama Kinafanyiwa Mchakato kuhakikisha kina kuwa sio tatizo tena! mfano ni Hii Barabara ya Rukwa Mbeya Nimiaka Hata minne haija Fika tangu ijengwe kwa Kiwango cha Lami... Jambo ambalo sijawahi Fikiria kurishuhudia,Nilijua itawezekana Wajukuu wangu ndio watakuja kuiona Lami hii Lakini Leo hata mimi Ninatembea Juu ya Lami! Sehemu ambayo ilikuwa ikitugharimu Siku nzima Leo Tuna Tumia Masaa Matano tu kwa Usafiri wa Umma.

Gari yetu ina korofisa Kidogo Mwendo wa Nusu saa tu kutoka Hapa Tulipo Unafika Tunduma
Tatizo Lime Rekebishwa Tiari tuna Ruhusiwa Kuanza Safari yetu
Tuna ipita Stendi ya Tunduma Mida yapata Saa Nne,kuanza kuitafuta Mbeya Jiji
Mzani wa Chapwa Tunduma Upo Maeneo haya
   Yapata Mida ya Saa Tano;Nikiwa Nimesha Fika Nyumbani Nina Kula Supu ya Mlowo;Mbeya

Maelezo ya wale Wazee yaliendelea Pamoja na kuwa onesha Changa moto tulizo nazo walikili kuwepo changamoto Lakini Wakanisihi Bora Leo Mnazungumzia Hizi Changa Moto Wenzenu Zamani Tulikuwa Tuna Zungumzia Matatizo! Mwanangu elewa kuwa Tatizo ni zaidi ya Changamoto! Tunajua Hoja zako niza kwenye Magazeti,Inaonekana Unajisomea sana Magazeti kijana ndio Faida yenu Siku Hizi,Nirahisi kupata habari na Habari Zime kuwa nyingi Mno kiasi kwamba inahitaji Uwe Makini ili Kujua Uhalisia na Porojo... Wengi Wanao Toa Habari wanatengeneza ama wana kuwa Wametumwa,Unategemea Habari Zinazo ufikia Umma Zita kuwaje? Nina jitahidi kueleza kadri ya Uwezo wangu lakini inaonesha wazi ninaeleza nusu ya kile wanacho kifahamu wao! Alisema Mzee Mmoja.
Haya wanayo Nieleza hawa wazee sio Hadithi nimeyashuhudia mwenyewe na Safari inaendelea.
Pia Wengi wanao ielezea Tanzania Hata Dra es Salaam yenyewe walifika miaka Kumi iliyo pita;Lakini ndio hao wana ielezea Vema Tanzania Wakati wao wana ishi nje ya nchi na wanapo Fika nchini wanaishia Kwenye Nyumba za Wageni na Uwanja wa ndege! Unategemea Mtajulishwa haya?


Inawezekana hawa wazee ni Makada wa Chama Tawala... Lakini Sio kweli kwamba wana Nihadaa Wana nieleza Ukweli... Wanatamani Niwe Shuhuda! Ingawa Mpaka Ninashuka Stendi Hatuja fanikiwa kufahamiana kiundani na hakuna aliye kumbuka kumuuliza Mwenzake jina,kwani Lugha ilikuwa Moja KISWAHILI na Ukisha Sikia Kiswahili Unajua wazi kuwa huyu ni Mwenzangu,huyu ni Mu Tanzania!
 Naam;Tembea Ujifunze Zaidi! Tembea Uone! Tembea Ndani ya Nchi Yako TANZANIA.
Namaliza kwa Kumu Shukuru Mwenyezi MUNGU Kwa Kunifikisha Salama.Hayo ndiyo niliyo kutana nayo Katika Safari yangu ya masaa Matano Kutokea Sumbawanga hadi Mbeya!

MJUMBE Sr
MBEYA

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top