Unknown Unknown Author
Title: MAYA ANGELOU AFARIKI DUNIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Maya Angelou, mshairi mashuhuri, mwandishi na mtetezi wa haki nchini Marekani amefariki akiwa na umri wa miaka 86. Angelou aliyepat...
Maya Angelou
Maya Angelou, enzi za uhai wake. Picha imepigwa November 3, 1971.
Maya Angelou, mshairi mashuhuri, mwandishi na mtetezi wa haki nchini Marekani amefariki akiwa na umri wa miaka 86.
Angelou aliyepata umaarufu katika miaka ya 1970 kwa kitabu chake cha "I know why the caged bird sing" alifariki huko Winston-Salem katika jimbo la North Carolina nchini Marekani.
Alizaliwa huko St.Louis , Misouri na alilelewa katika jimbo la Arkansas. Baada ya kubakwa akiwa mdogo aliacha kuongea kwa muda wa miaka mitano. Baadae katika maisha yake alifanya kazi mbalimbali kama vile mhudumu wa hoteli, mpishi na pia kondakta kwenye mabasi.
Maya hakupoteza upendo wake wa sanaa, muziki, uigizaji na dansi. Uandishi wake ulianza wakati ambapo mwandishi mmoja maarufu, m-Marekani mweusi James Baldwin aliposikia mambo aliyoyapitia Maya akiwa bado mdogo na kumhimiza aandike kitabu.
Mwaka 1993 aliyekuwa Rais wa Marekani, Bill Clinton alimuomba bi.Angelou aandike shairi lililosomwa katika sherehe za kuapishwa kwa Clinton kuwa Rais wa Marekani.(Martha Magessa)
CHANZO:VOA

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top