Bomu la kutupwa kwa mkono lauwa na kujeruhi wengine saba zanzibar
Wakaazi
wa Zanzibar wako katika hali ya wasiwasi baada ya kushuhudia tukio
lengine la kuripuka bomu kwa viongozi wa dini huku safari hii likiua
kijana mmoja na kujeruhi saba.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa upelelzi na makosa ya jinai zanzibar
Sacp Yussf Ilembo ameseme bomu hilo la kutupwa na mtu au watu
wasijulikana ambao walikuwemo ndani ya gari lilkuwahalina namba za
usajili lilitupa bomu hilo kwa kikundi cha wananchi waliokuwa pamoja na
viongozi wa dini amabo walikuwa wametoka msikitini na wamesimama nje ya
gari ndipo walipotupiwa bomu hilo na kijana mmoja Mohamed khatibu
Mkombalaguha ambaye ni mkaazi wa pongwe tanga aliyekuja Zanzibar kwa
ajili ya hitima kufariki hapo hapo na wengine saba akiwemo Sheik Kassim
Mafuta kujeruhiwa huku jeshila polisi hadi sasa hawajakamata mtu
yeyote.
Nao baadhi ya majeruhi Ahmed Haidar na mwanawe khalid Ahmed
wakiongea na ITV wakiwa wamelazwa hosptali ya Alrahma wamesema hawajui
wala hawakumuona mtu ailyerusha bomu hilo wao wameshtukia mripuko
mkubwa wakati wa saa mbili na nusu na kurushwa.
Hakuna taarifa yeyote iliyotolewa na seriklai wakati hili likiwa ni
tukio la pili la kuripuka mabomu kutokozea hapa zanzibar katika kipindi
cha miezi mine bada ya mezi wa februari mabomu zadi ya matatu kuripuka
katika mgahawa wa mercury na mabomu mawili nje ya lango kuu la kanisa la
angilkana mkunazini na hadi sasa hamna mtu aliyekamatwa.
Post a Comment