Unknown Unknown Author
Title: HABARI NJEMA:WAKATI TIARI KUNA TAARIFA YA MGOMO WA VYUO VIKUU VYOTE NCHINI;RAIS WA BUGANDO APATIKANA AKIWA HOI NA HAJITAMBUI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HIKI NDICHO KILIKUWA KINA ENDELEA..... Gwamaka Mbughi TAFADHARI MREJESHENI RAFIKI YANGU MDEDE AKIWA SALAMA Ni siku ya 4 sasa Ra...
HIKI NDICHO KILIKUWA KINA ENDELEA.....

TAFADHARI MREJESHENI RAFIKI YANGU MDEDE AKIWA SALAMA
Ni siku ya 4 sasa Rafiki yangu,Raisi wa Chuo cha Bugando na Pia Mwenyekiti /Raisi wa Shirikisho la vyuo vikuu Tanzania ie TAHIRISO hafahamiki alipo baada ya kupotea katika mazingira yenye utata sana.
Kama hizi ndio siasa za Bongo basi mwelekeo wake ni Mbaya sana, na Ujumbe huu uwe kwa Wanavyuo wote

Ndugu mwanachuo wa CUHAS
Sote tuna taarifa ya kutokuonekana kwa kaka yetu mpendwa na Rais wetu wa serikali ya chuo lakini pia Mwenyekiti wa vyuo vikuu vya Tanzania (TAHILISO)
Ni majonzi na simanzi makubwa kwetu sote
Ni nia na dhamira yetu kuhakikisha tunampata akiwa katika hali yeyote.
Kwanza vyombo vya dola vinafanya jitihada mkubwa sana kumtafuta.
Pili na sisi tuonyeshe hisia zetu kuhakikisha tunampata tukishirikiana na vyuo vikuu vyote TZ
Tatu tunaomba mchango wako wa HALI na MALI
Leo kuanzia saa nne tujitokeze sote kwa umoja wetu kuhudhuria press conference itakayofanyika maeneo ya chuoni...Tutajiunga na wanafunzi wa SAUTI...Tofauti zetu tuweke pembeni..Musa Mdede zaidi tu ya kuwa rais na mtetezi wetu lakini pia ni binadamu kama ww na mimi..Hatutegemei ubaki ndani bila kujitokeza kushauriana na wenzako...
Mungu Atusaidie
Viva cuhaso viva

HABARI NJEMA....!


pichani ni Mdede kabla hajatekwa


RAIS WA BUGANDO APATIKANA USIKU HUU
akutwa akiwa katupwa Usagala
Akiwa hajitambui na akiwa amepoteza kumbukumbu


Rais wa chuo kikuu Bugando Mussa Leonard Mdede amepatikana usiku huu akiwa hajitambui na amepelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando kwaajili ya vipimo na matibabu zaidi,bwana Mdede ambaye pia ni mwenyekiti wa TAHILISO nchini alitoweka tangia tarehe 18 mwezi huu saa kumi jioni,na haikuweza kufahamika mara moja yupo wapi na kama ametekwa nani kamteka, mpaka usiku huu taarifa za kupatikana kwake zilipotufikia.

Akiongea na mwandishi wa habari hii,waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Bugando Benjamini Thomas,alisema Mdede aliletwa na vijana watatu,wanaume wawili na mwanamke mmoja waliodai kumuokota bwana Mdede katika eneo la Usagala akiwa hajitambui wala kujielewa,anaendelea kusema kwa mujibu wa mama mwenye Nyumba wa Mdede,watu hao walidai baada ya kumuokota jana usiku katika eneo hilo la Usagala,waliamua kumchukua na kwenyda kumuhifadhi katika eneo la Igoma, alipoanza kupata fahamu na kueleza anaishi wapi ndipo wakamleta nyumbani kwake,huku watu hao wakidai walishindwa kumleta jana na asubuhio kutokana na Mdede kutojitambua na kuwa katika hali ya kupoteza kumbukumbu,hata hivyo mama  mwenye nyumba  anasema watu hao hawakukaa sana wakaondoka bila kutoa maelezo zaidi.

Waziri mkuu huyo wa Bugando aliendelea kusema,"kwa mujibu wa mama mwenye nyumba,alisema kwamba mara baada ya watu hao kumleta nyumbani hapo wakiwa wamempakia kwenye gari aina ya Kenta,walitoa maelezo machache na hawakutaka kukaa sana wakaaga wakaondoka ",mwandishi wa habari hii alipotaka kujua kwamba ni  mtu gani alikuwa wa pili kupata taarifa hizo kabla  ya yeye waziri mkuu,alisema ni kaka zake Mdede na ndugu zake wengine,alisema mmoja wa kaka yake Mdede anayefanya kazi katika moja ya bank iliyopo jijini hapa,alipata taarifa za kupatikana kwa mdogo wake akiwa kazini,lakini alinyimwa ruhusa ya kuondoka kazini mpaka pale alipolazimisha kuondoka,anaendelea kusema kaka yake Mdede alipofika kwenye Nyumba aliyopanga Mdede alimkuta mdogo yake akiwa hajielewi wala kujitambua japo hakuwa na jeraha lolote mwilini.

Kwa mujibu wa waziri mkuu Thomas anasema kaka yake alijaribu kuwapigia mara kadhaa lakini yeye hakupokea simu yake kwakuwa alikuwa anatoa tamko kwa waandishi wa habari juu ya kupotea kwa Mdede,na walipomaliza kutoa tamko walielekea kwa Mdede baada ya kuambiwa na kaka yake kila kitu,"na tulimkuta anamwonekano, anahali dhoofu,akiwa anaongea kwa tabu na huku akiwa hana kumbukumbu nzuri zaidi ya kumbukumbu ya kabla hajatekwa"anaendelea kusema waliwasiliana na mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Nyamagana na wakakubaliana wasitoe taarifa kwanza mpaka watakapo muhoji na kuangalia taratibu zingine za kiulinzi,na baadae ndipo walipojiridhisha na kuamua kumpeleka hospitalini Bugando kwani awali alikuwa akipatiwa matibabu palepale nyumbani kwake,lakini waliamua kumpeleka hospitali hiyo kwa ajili ya vipimo na uchunguzi zaidi na hasa walipoona hali ya Mdede haieleweki na wakahisi huenda akawa amelishwa vitu vibaya kama sumu.

Mpaka sasa bwana Mdede hana kumbukumbu na hajui kipi kilichomtokea na wala hajui alikuw awapi.

Blog hii ya MJUMBE BLOG ,itaendelea kuwaletea taarifa zaidi na picha kadili tutakavyokuwa zinatufikia na kwa sasa Mdede amelezwa hospitali ya rufaa Bugando Mwanza.
Asante:Nicholaus Kilunga

 
MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top