Shughuli zinafanywa leo kukumbuka tukio la karne kamili iliyopita mjini
Sarajevo, ambapo mrithi wa mfalme wa mamlaka ya Austria-Hungary
aliuliwa na mzalendo wa Serbia na kuwa chanzo cha kuzuka Vita vya Kwanza
vya Dunia.
Vilembwe vya prince huyo, Franz Ferdinand, watahudhuria gwaride litalofanywa katika kasri yao karibu na Vienna, Austria.
Princess Anita Hohenberg, kilembwe cha Franz Ferdinand, aliiambia BBC kwamba Franz Ferdinand daima hakupenda vita:
"Baba wa babu yangu angeshtushwa, angeshtuka kabisa, kwa sababu akijua upungufu wa jeshi lake, kwa sababu alikuwa mkuu wa jeshi.
Vita hivo vilikuwa vibaya, vibaya sana."
Austria sasa haina mfalme.
Credit: BBC.
@Sr
Post a Comment