Mishumaa 16 imewashwa na shada la maua ktk kumuenzi mtoto RUKIA.
Mtoto Rukia Abdalah alizaliwa 2010 ktk kijiji cha Namkonjela Ruangwa Lindi Tanzania.
Akiwa na umri wa miaka mitatu(2012) aliungua kwa maji ya moto ktk kifua mpaka ktk sehemu za siri,ilichukua siku kadhaa kumfikisha hospital ya wilaya.Alipofikishwa hospital alipokelewa na kupewa rufaa ya kwenda hospital ya Ndanda au Nyangao.
Wazazi hawakuwa na uwezo wa kifedha,mtoto aliteseka kwa kukosa huduma kwa siku 33 huku akiwa ameanza kuoza na kutoa harufu.
Katika matembezi yangu yasiyo na ukomo nilibahatika kuiona shida hii tarehe 2June 2012 na kujitwisha dhamana ya kupigania uhai wake.
Nilipost fb kuomba msaada wa fedha niweze kufika hospitali pasipo kujali nitaitwa tapeli au jina jingine tofauti na nia yangu,nakumbuka 4June 2012 nilimfikisha Nyangao hospital kwa msaada wa wasamalia wema kunitumia pesa.
Mtoto alipata tiba na kuanza kupona huku akiwa ameanza kurejesha sura ya matumaini na kuona nuru ya uzima,aliwapenda sana madaktari wake na kuwaita akina shangazi.
Mtoto huyu alidumu kwa siku 11 tu hospitali na akapatwa maralia ghafla akaiaga dunia tarehe 15 June 2012 saa 12:30 jioni.
Nilifuata mwili wa marehemu RUKIA siku ya pili tayari kwa mazishi kijijini kwao Namkonjela kilometre 86 toka Nyangao.
RUKIA alizikwa tarehe 16 June 2012 saa 11:30 jioni.
Siku ya Mtoto wa Afrika.
TUNAKUKUMBUKA DAIMA.
Ndugu zangu kwa kujali thamani ya mama na mtoto ndiyo maana nimetumia muda wangu na kipato changu kusafiri umbali mrefu niwafundisha watoto kujitambua na kuwapa maarifa ya kujikomboa ktk matatizo yao.
Safari hii nimesindikizwa na mtoto Shabani ambaye nilimuokoa ktk tatizo la upofu niliyemshika mkono wangu wa kuume(pichani),hakujali kuvaa viatu wala kunywa chai alisema TWENDE WOTE.
(Habari zaidi Google Mtoto Rukia usome).
Afrika ni ya Waafrika,Waafrika ni sisi sote.
Hakuna mwafrika mwenye haki ya kupata zaidi ya kupata Waafrika wote.
WATOTO WA AFRIKA NI WETU SOTE.
#TAFADHARI:
Share Ujumbe Huu Kwa Marafiki,ndugu na Jamaa ili Nao Wajifunze Jambo Kisha Andika Neno RIP RUKIA.
MJUMBE Sr

Post a Comment