Afya wa Lwakatare yaendelea kudorora,alazwa MOI
![]() |
| Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, jana, kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya Shingo. |
Lwakatare ambaye anasumbuliwa na maumivu ya shingo
yaliyosababishwa na kusagika kwa pingili mbili za shingo alifika
hospitalini hapo Jumanne ya wiki hii, baada ya kuzidiwa na maumivu usiku
wa kuamkia siku hiyo.
Akizungumza wodini hapo jana alisema alikuwa
anasubiri ripoti ya madaktari ambao walikaa kikao cha kujadili tatizo
lake na jinsi ya kulitatua hatua za awali zilizochukuliwa na kikao hicho
ni kuhamishiwa kitengo cha mifupa Moi.
“Walivyokuja asubuhi(jana) baada ya kikao
walinihamisha wamenileta huku na nimekabidhiwa daktari ambaye amepewa
aniangalie na nimekabidhiwa namba yake hapa niwasiliane naye ndiyo
nitajua nini kitaendelea huku,”alisema Lwakatare.
Alisema kwa sasa bado anasikia maumivu kwa mbali
japokuwa amefungwa kifaa maalumu cha kuifanya shingo inyooke na kuzuia
isichezecheze.
Katika uchunguzi uliofanywa juzi na madaktari
ulionyesha kuwa hakuna njia zaidi yakuweza kumsaidia kupunguza maumivu
hayo kama hatofanyiwa upasuaji wa kurekebisha pingili hizo.
“Hakuna kitu naogopa kama operesheni wakati ule
ilikuwa pingili ya sita na ya saba ila sasa ni ya tatu na ya nne na
nilishindwa kufanyiwa operesheni kipindi hicho kwa sababu niliona
nikifanyiwa operesheni itanilaza na nitapoteza muda ila kwa sasa sina
jinsi,”

Post a Comment