Unknown Unknown Author
Title: MIUNDO MBINU,ILIMO,AFYA,ELIMU ZATENGEWA BAJETI KUBWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
...


Serikali imetangaza kuongeza bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2014/15 kutoka Sh. trilioni 19.6 hadi Sh. trilioni 19.853 huku ikielekeza kiasi kikubwa cha fedha katika sekta za afya, elimu, miundombinu na kilimo.
Aidha, kiasi kingine kikubwa kimetengwa kwa ajili ya kuimarisha utawala bora.
Akiwasilisha bajeti ya serikali bungeni jana, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salumu, alisema kuwa kati ya fedha hizo, Sh. trilioni 13.4.8 zitakuwa ni za matumizi ya kawaida wakati Sh. trilioni 6.445 zitaelekezwa katika maendeleo.
Mkuya alieleza kuwa sekta ya nishati imetengewa Sh. trilioni 1.09 huku Sh. bilioni 290.2 zikitengwa kwa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini na Sh. bilioni 151 kukamilisha ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Waziri huyo alisema sekta ya miundombinu na usafirishaji imetengewa Sh. trilioni 2.109. Kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 170  zitatumika kununulia mabehewa na ukarabati wa reli ya kati na Sh. trilioni 1.415 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja.
Sekta ya kilimo kwa mujibu wa Mkuya, imetengewa Sh. trilioni 1.085 kwa ajili ya kuimarisha miundombinu na umwagiliaji.
Waziri Mkuya aliliambia bunge kuwa sekta ya elimu  imeongoza kwa kutengewa bajeti kubwa ya Sh. trilioni 3.465 na kuwa Sh. bilioni 307 zimetengwa kugharamia mikopo ya elimu ya juu.
Sekta ya maji imetengewa Sh. bilioni 665.1 kwa ajili ya kuimarisha miundombinu  na maji mijini na vijijini ikiwa ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa visima katika vijiji 10 kwa kila halmashauri na kukamilisha kwa ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu Chini hadi Dar es Salaam.
Wizaya ya Afya imetengewa Sh. trilioni 1.588 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, kuzuia magonjwa ya mlipuko, chanjo za watoto, ujenzi wa zahanati na kudhibiti Ukimwi na malaria.
Waziri Mkuya alisema kuwa vile vile Sh. bilioni 579.4 zimetengwa kwa ajili ya kuimarisha utawala bora iikijumlisha kugharamia Bunge Maalum la Katiba; vitambulisho vya Taifa; uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014; kuhuisha daftari la wapiga kura, maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015; mapambano dhidi ya rushwa na utoaji wa haki kwa wakati.
 
 NIPASHE
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top