Na Hudugu Ng'amilo
Makamu
Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa ametoboa
siri ya chama hicho kung'ang'ania Muungano serikali mbili akisema hiyo
ndiyo sera yake pekee iliyopitishwa na wanachama wake wote kwa kura ya
maoni.
Msekwa alieleza hayo katika mahojiano maalumu na wahariri wa gazeti hili yaliyofanyika nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam.
Msekwa
ambaye katika habari iliyochapishwa na gazeti hili jana alieleza kuwa
binafsi, hana tatizo na suala la idadi ya Serikali katika Muungano,
alisema kamwe hawezi kukishauri chama chake kukubaliana na mapendekezo
ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya
muundo wa serikali tatu.
"Siwezi
kuishauri CCM kukubali serikali tatu. Hili la Serikali mbili ni sera ya
CCM, siyo tu sera ya kawaida, bali hii ni sera pekee iliyopitishwa na
wanachama wote kwa kura ya maoni," alisema Msekwa ambaye pia ni Spika
mstaafu wa Bunge.
Alisema
tofauti na sera hiyo ya serikali mbili, sera nyingine za chama hicho
huanzia katika ngazi ya Kamati Kuu, kujadiliwa na Halmashauri Kuu ya
Taifa (Nec) na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.
Msimamo ulikoanzia
Kiini cha
sera hiyo kutengenezewa utaratibu maalumu, kilitokana na sakata la
Kundi la Wabunge 55 (G55), kuanzisha agenda ya kutaka Serikali ya
Tanganyika ndani ya Muungano na hatimaye Bunge kupitisha Azimio la
kuanzisha serikali hiyo.
Msekwa
ambaye wakati huo alikuwa Naibu Spika lakini akiongoza Bunge kutokana na
aliyekuwa Spika, Chifu Adam Sapi Mkwawa kuwa mgonjwa, alisema ushauri
wa kurudi kwa wanachama wa CCM kuwauliza wanataka serikali ngapi
ulitolewa na Mwalimu Julius Nyerere.
Itakumbukwa
kuwa hatua ya Bunge kupitisha azimio hilo la kuanzisha Serikali ya
Tanganyika ilimkera Mwalimu hadi akatunga kitabu, Uongozi Wetu na Hatima
ya Tanzania akiwashutumu aliyekuwa Waziri Mkuu, John Malecela na
aliyekuwa Katibu Mkuu wa (CCM), Horace Kolimba. "Mwalimu alitueleza
kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa, kuwa Bunge limekwishapitisha azimio na
likipitishwa ni lazima litekelezwe na Serikali. Alisema mkikataa azimio
la Bunge hivihivi mtaleta mgongano wa kikatiba, msiamue peke yenu,
nendeni kwa wanachama wote muwaulize ili uamuzi uwe wa wote," alisema.
Alisema
kutokana na ushauri huo, mwaka 1993 CCM iliandaa na kusimamia upigaji
kura za siri za maoni katika kila tawi, wanachama wakitakiwa kujadili na
kuchagua kati ya serikali moja, mbili au tatu.
"Matokeo
yalipofika katika Halmashauri Kuu, ilionekana wanachama walio wengi
katika matawi mengi walitaka serikali mbili, na hapo ndipo ikapitishwa
sera ya serikali mbili," alisema na kusisitiza
soma zaidi mwananchi.
Post a Comment