Mbunge wa
Temeke, Abbas Mtemvu akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi
ya CCM, wilaya ya Temeke, leo katika ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo
jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa
Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, akimkabidhi hati ya
pongezi , Zaitun Lukinga, ya kuwa kiongozi wa Jumuia ya Wazazi awamu
zaidi ya moja katika nafasi ya Katibu wa Jumuia ya wazazi Kata ya
Kurasini, wakati wa mkutano huo leo
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo. Habari Picha na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog(P.T)
NA BASHIR NKOROMO, TEMEKE
MBUNGE wa Temeke Abbas Mtemvu amewananga wapinzani akisema hata wakisimamisha mgombea mmoja mmoja, katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, CCM itawabwaga.
MBUNGE wa Temeke Abbas Mtemvu amewananga wapinzani akisema hata wakisimamisha mgombea mmoja mmoja, katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, CCM itawabwaga.
Amesema,
uhakika huo anao na hata wapinzani wenyewe wanajua hilo, kwa kuwa
hawaizidi CCM kwa weledi wa kisiasa, kwa akili wala wingi wa wanachama.
Mtemvu
amsema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi
Wilaya ya Temeke, kilichofanyika leo, Juni 27, 2014, kwenye Ukumbi wa
Manispaa ya wilaya hiyo, mjini Dar es Salaam.
"Wapinzani
baada ya kuona kuwa hawatuwezi kwa kila chama kivyake, sasa mnaona
wanavyotapatapa, mara eti huo Ukawa walioanzisha wanataka pia kuutumia
kwenye chaguzi, kuweka mgombea mmoja mmoja kwa wote, mimi bado naamini
hata wafanyeje CCM itawabwaga tu", alisema Mtemvu.
Mtemvu
alisema, pale ambapo wapinzani wamekuwa wakipenya na kunyakuwa ubunge au
udiwani ni pale ambapo CCM wenyewe wanakuwa wamejichanganya.
"Ikifika
acheni mambo ya kuanza mizozano ya ndani kwa ndani kutokana na makundi
ambayo husababishwa na baadhi ya wagombea au wanachama wanaowataka
wagombea kwa lazima, tukiachana na hili nawahawakikhieni wapinzani
hawapati hata kiti kimoja cha cha mtaa", alisema Mtemvu.
Mtemvu
aliwataka wana-CCM pia kuachana na mambo ya kushughulika tu na wanaotaka
nafasi ambao wana fedha, akisema, kufanya hivyo kunasababisha baadhi
kuwa wagombea kutokana na uwezo wa fedha tu na siyo wa uongozi.
Aliwataka
mtu anapowajia kwa fedha kuzipokea na kuzila, lakini wakati
waanapofikia maamuzi muhimu kwenye uchaguzi wahakikishe wanachagua yule
wanayemfahamu kwa thati kwamba anao uwezo wa uongozi.
Alisema,
wapo baadhi ya wanachama wa CCM wanao uwezo wa kuongoza lakini hawana
fedha, hivyo watu wa aina hiyo wasitoswe kwa sababu ya ufukara wao.
Mtemvu
alisema kiongozi mwenye uwezo ni yule anayekubalika na watu, saa zote
yupo na watu na anajali maslahi ya wanyonge siyo wale anaowajua kuwa ni
wake tu.
"Mfano ni
kama hivi tunavyofanya sasa wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam. Kila mara
tunapigania wanyonge, juzi nimepambana kuwatetea mamalishe wasifukuzwe
hovyo, japo baadhi ya watu tena waliopewa malmaka na Rais waknibeza eti
nina maslahi binafsi, khaa, yaani mimi niwe na maslahi na mamalishe huu
kama siyo uzushi ni nini?" alisema Mtevu.
MJUMBE Sr
Post a Comment