Unknown Unknown Author
Title: MWANAMKE MWINGINE ABAKWA NA KUNING'INIZWA JUU YA MTI INDIA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 19 amekutwa amening’inizwa juu ya mti katika kijiji kimoja Kaskazini mwa India, likiwa ni tu...




India
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 19 amekutwa amening’inizwa juu ya mti katika kijiji kimoja Kaskazini mwa India, likiwa ni tukio la tatu kutokea ndani ya wiki moja katika Jimbo la Uttar Pradesh.
Mwili wa mwanamke huyo umekutwa katika eneo la Moradabad ambapo familia yake imewaambia polisi kuwa alibakwa huku uchunguzi wa madaktari ukiendelea kufanyika.
Mwanamke mwingine alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika Jimbo la Uttar Pradesh siku ya Jumatano.
Mwezi uliopita mabinti wawili wadogo walibakwa na kundi la watu katika mazingira kama hayo na kuibua maandamano ya hisia kali nchini India.
indiateen
Siku ya Jumatano, mwanamke mwenye umri wa miaka 44 nae alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika eneo la Bahraich.
Polisi wamesema kuwa alikuwa akipatiwa vitisho na wanakijiji kwa kuuza pombe katika eneo hilo na familia yake ilifungulia kesi watu watano kuhusiana na kifo hicho.
Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza >>>LIKE Kwenye Page Yetu Kushoto Chini ya Blog Yetu ya MJUMBE BLOG au Ingia MJUMBE BLOG mara kwa mara ili Upate Picha,Matukio na Matangazo Mbalimbali.

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top