Henry Joseph
KLABU ya
Simba imetangaza rasmi kuachana na nyota wake wanne ambao mikataba yao
imefikia tamati na tayari imewaambia watafute maisha sehemu nyingine.
Wachezaji
hao waliofungashiwa virago ni Haruna Shamte, Henry Joseph, Ramadhan
Chombo ‘Redondo’ pamoja na Uhuru Seleman lakini kuna wengine ambao wapo
mbioni kuachwa.
Hatua
hiyo imetokana na klabu hiyo kwa sasa kutokuwa na uhakika wa kufanya
usajili katika siku za hivi karibuni kutokana na kutokuwepo kwa viongozi
watakaosimamia zoezi hilo, hali iliyoufanya uongozi wa klabu hiyo
kufikia hatua hiyo.
Ramadhan Chombo ‘Redondo’
Kaimu
Makamu Mwenyekiti wa Simba ambaye anamaliza muda hivi karibuni, Joseph
Itang’are ‘Mzee Kinesi’, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, wachezaji hao
ni bora wakatafute maisha sehemu nyingine kwani wakiendelea kusubiria,
mambo yanaweza kwenda ndivyo sivyo.
“Mpaka
sasa haijulikani ni lini watapatikana viongozi wapya watakaosimamia
zoezi zima la usajili, maana mchakato wa kuwapata viongozi umezongwa na
matatizo mengi na juzi tu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi ametangaza kuusimamisha.
Ramadhani Haruna Shamte.
“Watakaoangaliwa
zaidi ni wale wenye mikataba kwa sababu hata kama wataachwa, watakuwa
na uhakika wa kulipwa, hivyo kwa wale ambao mikataba yao imeisha, ni
bora wakatafuta sehemu za kwenda,” alisema Mzee Kinesi na kuongeza:
“Wakati michuano ya ligi kuu msimu uliopita ilipofikia tamati, tulikaa kikao na wachezaji na kuwaambia uongozi wetu ambao unamaliza muda wake hautafanya usajili utakaohusika, jambo hilo litawahusu wale watakaoingia madarakani
Post a Comment