Unknown Unknown Author
Title: PICHA NA MAELEZO:PONGEZI WAHUSIKA WA USAFI KATIKA MJI MDOGO WA MLOWO:DAMPO LA SOKO KUU LIME KUWA SAFI;LAKINI.....!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Picha Gari la Kukusanya Taka Ngumu Likikatiza Katika Mji Mdogo wa Mlowo,Mbeya wiki iliyo pita. Picha Mbili za Hapo Juu Zina Onesha H...
Picha Gari la Kukusanya Taka Ngumu Likikatiza Katika Mji Mdogo wa Mlowo,Mbeya wiki iliyo pita.

Picha Mbili za Hapo Juu Zina Onesha Hali ya Dampo la Soko kuu ilivyo kuwa hapo awali



Huu Ndio Mwonekano wa Dampo la Soko kuu la Mlowo kwa sasa kama lilivyo kutwa na Mshika Kamera Wetu siku kadhaa zilizo pita.

Lakini...
Mdau wa MJUMBE BLOG Alipo katika Mizunguko yake ya kila siku ndani ya Mji mdogo wa Mlowo amegundua Kuwepo kwa Utamaduni mpya miongoni mwa wakazi wa Mlowo walio amua Kutafuta njia ya mkato na kuanza kumwaga Taka za Majumbani kwao Kando kando mwa Mto Mlowo.Hili Una weza ukalishuhudia kama Uta elekea Upande ilipo Shule ya Nalyele,Kuna sehemu ya Mto inayo fahamika kama Bichi! Huku Kamera Yetu ili shuhudia Milima ya Mabaki ya Taka Ngumu iliyo Jipanga na Kusambazwa kando kando ya Mto huo ilisubiri Msimu wa Mvua Ufike ili Isafirishwe Kuelekea Huko kusiko Julikana!
Karibu hapa nawewe Ushuhudie Milima hiyo....
Picha ikionesha Milima iliyo tokana na Umwagaji wa Taka ulio kithiri kandokando ya Mto Mlowo
Picha Nyingine
Picha Zaidi Ikionesha Mabaki ya Vioo na Chupa zilizo vunjika zika telekezwa kando ya Mto Mlowo
Mabaki ya Baadhi ya Nywele kutoka kwa Vinyozi wa Mji Mdogo wa Mlowo kama yalivyo kutwa na Kamera yetu.

Tuna Shukuru Uongozi wa Mji mdogo wa Mlowo;Lakini tuna endelea kuukumbusha kuwa Binadamu au jamii yetu inafanya kila jitihada kuhakikisha inapunguza taka majumbani mwao lakini bado haija Tengewa maeneo ya Kumwagia Taka Kila Mtaa.Hivyo Basi Rai yetu kama Sehemu ya Jamii husika Tuna Omba Pindi Taarifa hizi zitakapo wafikia Mujaribu kuliona hilo kwa jicho la Pekee kama mlivyo liona la Soko kuu.
Tuna amini kama kila mtaa utakuwa na Sehemu yake ya kumwaga Taka Mji wa Mlowo Unaweza kubaki Mahali safi Salama kwa afya misimu yote.
Tuna Tanguliza Shukrani za Dhati;Asante.
Wenu Katika Ujenzi wa Jamii Mpya Mdau wa MJUMBE BLOG!

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top