KWA MARA YA KWANZA NDEGE YA @FASTJET YARUSHWA NA MAARUBANI WATANZANIA.
Jina la fastjet sio geni Tanzania na hii ni kutokana na kuzidi kukua
kila siku kutokana na huduma inayotolewa kusafirisha abiria kutoka kona
kadhaa za Tanzania kwa kuzingatia muda na bei nafuu pia.
Good news
ni kwamba shirika hili la ndege ambalo limekua likisafirisha abiria wa
ndani ya nchi kati ya Dar es salaam na Mwanza, Mbeya na Kilimanjaro kwa
sasa, limeanza kuwapa shavu marubani Watanzania.
Kwa mara
ya kwanza Marubani Watanzania Arif Jinah na William Zelothe wameirusha
ndege ya abiria ya Fastjet A319 mpaka Mwanza wakiwa wamezingatia viwango
vya usafirishaji vya kimataifa ambapo marubani hawa wako kwenye idadi
ya Marubani zaidi ya kumi Watanzania walioajiriwa na fastjet.
Siku
zote wafanyakazi ndani ya ndege na kwenye ofisi zao ni Watanzania kwa
asilimia kubwa ila Marubani ndio hawakuwa Watanzania.
Unaambiwa
fastjet ilipoanza kufanya kazi Tanzania ilikosa marubani wanaoweza
kuendesha ndege aina ya Airbus na ndio maana hii ni good news manake
Watanzania wa kwanza wameweza kufuzu na kuendesha ndege wao wenyewe.
Hongera sana kwa rubani Arif Jinah na William Zelothe.
Endela Kututembelea Mtandaoni Kwa Kuandika Neno MJUMBE BLOG ili Uhabarike Zaidi na Upate Picha na Matukio Mbali mbali yanayo Jiri nchini.
Home
»
»Unlabelled
» PICHA NA MAELEZO:UNA AMBIWA HAWA NDIO MARUBANI WA KITANZANIA WALIO RUSHA FASTJET KWA MARA YA KWANZA!
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment