Unknown Unknown Author
Title: PICHA:BAADA YA SOKO LA KARUME KUUNGUA JANA USIKU:NI VILIO,SIMANZI NA HUZUNI KUBWA KWA WAFANYABIASHARA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa na mabanda yao katika soko la Karume wakiwa na nyuso za majonzi mara baada ya mabanda yao kut...



Baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa na mabanda yao katika soko la Karume wakiwa na nyuso za majonzi mara baada ya mabanda yao kuteketezwa kwa moto mkubwa ulioteketeza sehemu kubwa ya mali za wafanyabiashara hao.
 Baadhi ya Wafanyabiashara na wakazi wa Jiji la Dar wakiwa katika soko la karume kujionea hali ilivyokuwa mara baada ya moto kuteketeza  kila kitu.
 Moto ukiendelea Kuunguza mabati na vitu mbalimbali katika Soko hilo la Karume, Jijini Dar Es Salaam
 Askari wa Kikosi cha Zima Moto akiendelea na Zoezi la kuzima Moto katika Soko la Karume lililoteketea kwa Moto ambao chanzo chake hakijulikani bado
 
Mmoja wa mfanyabiashara katika soko hilo hakikusanya mabati yake mara baada ya kuteketea kwa moto katika Soko la Karume
Wafanyabiashara wakikukasanya mabaki ya mabati mara baada ya mabanda yao kuteketea kwa moto uliowaka tokea usiku wa kuamkia leo katika Soko hilo la Karume.
Mfanyabiashara akiamisha baadhi ya mali alizoweza kuziokoa mara baada ya moto mkubwa kuteketeza soko la Karume.
Masanduku ya chuma yakiwa yameungua kabisa na moto mkubwa ulioteketeza sehemu kubwa ya Soko la Karume.
Wakazi wa Jiji la Dar Wakishuhudia jinsi kikosi cha Zimamoto kikiendelea na zoezi la Uzimaji wa moto huo ambao umeendelea kuteketeza mali za wafanyabiashara wa soko hilo.
Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
MJUMBE BLOG

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top