Wanachama na
Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho, wakipiga
kwata kuelekea Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa, jijini Dar es
Salaam, leo, kupeleka barua ya kumuomba Msajili huyo wa vyama, kuwataka
viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema kuzingatia Katiba ikiwemo kuitisha
kikao cha Baraza Kuu na kuzingatia matumizi bora ya fedha za Chama.
Mjumbe wa
Baraza Kuu Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya
Temeke Joseph Yona (kushoto) akiongoza wenzake kuingia Ofisi ya Msajili
wa Vyama leo kuwashitaki viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho kwa
kudaiwa kutotekeleza Demokrasia na kufuata Katiba ndani ya Chama
Yona akisaini
kitabu cha wageni kwenye kwenye mapokezi ya Ofisi ya Msajili wa Vyama
Jijini Dar es Salaam, alipowasili ya ujumbe wake. Kulia kwa Yona ni
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe
wa Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo
Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Nchini akimkaribisha Yona na msafara wake.
Wanachama
waliofuatana na wajumbe wa Baraza Kuu Chadema wakisubiri kuwasisha barua
yao kwa Mkuu wa Masijala wa Ofisi ya Msajili wa vyama.
Yona akionyesha abarua ambayo baadaye aliikabidhi masijala kwa ajili ya kumfikia Msajili wa vyama
Yona akikabidhi barua yao, kwa Mtunza kumbukumbu Mkuu wa Ofisi ya Msajili wa vyama, Jihadhari Saidi.
Yona akizungumza nje ya Ofisi ya Msajili baada ya kuacha barua yao kwa Msajili wa Vyama
Mwenyekiti
wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe
wa Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo akisoma
taarifa yao kabla ya kwenda kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
baadaya ya kutoka kwa Msajili ya vyama
Baadhi ya wanachama wanaodaiwa kuwa wa Chadema wakiwa na mabango nje ya Ofisi ya Msajili wa vyama
Eti Bora Chadema ife kuliko Mbowe kutapeli?
Chadema wakiomba msaada kwa Msajili wa vyama
Ujumbe mzito kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
Wanachama
na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho,
wakiwa nje ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo kupeleka
maombi ya kutaka Mkaguzi huyo wa Hesabu za serikali kufanya ukaguzi wa
hesabu wa Chadema kwa madai kwamba viongozi wa ngazi za juu wanazitafuna
VIJIMAMBO BLOG
Post a Comment