Mnenguaji wa Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis akionyesha sehemu alikopigwa risasi mbili mwilini na mtu aliyedaiwa ni askari polisi.
MNENGUAJI wa
Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis ambaye usiku wa Jumatano iliyopita
alipigwa risasi mbili mwilini na mtu aliyedaiwa ni askari polisi,
ameweka undani wa sakata hilo.Akizungumza na gazeti hili juzi nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, majeruhi huyo alisema tukio hilo lilijiri maeneo ya Mwananyamala- Kisiwani karibu na Ofisi za Chama cha Wananchi (Cuf) na kuongeza kuwa, kisa ni kubishana na askari huyo aliyetaka kuzimwa kwa matarumbeta kutoka kwenye kikundi chao kilichokuwa kikipita eneo hilo.
“Sisi tulikuwa tukipita na matarumbeta, askari wakatusimamisha na kutuamuru tuyazime kisha kutaka kutukamata watupeleke kituoni eti serikali imekataza.
“Tuliwaambia mbona ni mapema sana kwani ilikuwa saa kumi alasiri na Kova alisema ngoma za Kanga Moko, Kigodoro na nyingine zisipigwe usiku. Pia tuliwaambia tulichokuwa tukikifanya si ngoma hasa, ni matarumbeta tunapita kuwaalika watu kuwa leo kuna shughuli sehemu.
Mnenguaji wa Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis akiwa hoi kitandani baada ya kujeruhiwa na risasi.
“Baada
ya majibu hayo ndipo askari mmoja hakutaka hata kuendelea na
mazungumzo, alitoa bastola kiunoni na kunipiga risasi mbili, moja
kiunoni, nyingine kwenye mbavu halafu akapiga tena hovyo hewani risasi
zilizobaki. Kwa kweli nimeumia sana,” alisema Zawia.Mnenguaji huyo alisema kutokana na hali yake kuwa mbaya alipelekwa Kituo cha Polisi cha Mwinjuma na kupewa Polisi Fomu No. 3 (PF3) kisha kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni, Mwananyamala kwa ajili ya matibabu ambapo kwa mujibu wake alitolewa risasi mbili.
Baada ya kuzungumza na majeruhi huyo, waandishi wetu walikwenda kwenye Kituo cha Polisi Mwinjuma ambako ndiko alikoripoti PF3.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Dar, Camillius Wambura hakupatikana kwa simu juzi kuzungumzia.
MJUMBE Sr
Post a Comment