Waziri ya
Fedha, Saada Salum Mkuya jana aliwasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha
wa mwaka 2014, ambao umefuta misamaha ya kodi katika maeneo yaliyokuwa
yakilalamikiwa na watu wa kada mbalimbali nchini.
Katika
muswada huo Serikali imefuta misamaha ya kodi ya mapato inayotokana na
michezo kubahatisha na ukodishaji wa ndege nje ya nchi.
"Muswada
umependekeza waziri husika kutotoa msamaha wa ushuru wa mafuta kwenye
mafuta isipokuwa mafuta ya petroli yanayotumika kwenye miradi mbalimbali
inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo," alisema Mkuya.
Mkuya
alisema kuwa katika muswada huo, Serikali imeondoa saruji, nondo na
mabati katika orodha ya bidhaa zinazochukuliwa kuwa ni bidhaa za mtaji
ambazo kwa sasa hupata msamaha wa kodi kupitia Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC).
"Lengo ni
kuhamasisha uzalishaji wa saruji, nondo na mabati pamoja na kulinda
viwanda vya uzalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini dhidi ya ushindani wa
bidhaa za aina hiyo zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchi,"alisema
Mkuya.
Alisema
kuwa Serikali imefuta msamaha wa kodi ya mapato yanayotokana na
ukodishaji wa ndege nje ya nchi ili kupunguza misamaha isiyokuwa na
tija.
"Marekebisho
haya yanalenga kutoza mapato yanayotokana na ukodishaji wa ndege nje ya
nchi, badala ya kusamehe kodi ya mlipakodi asiye mkazi, ambaye hatimaye
hulazimika kulipa kodi itokanayo na mapato hayo nchini kwake,"alisema
Mkuya.
Marekebisho
hayo yanapendekeza kufuta misamaha ya kodi inayotolewa kwa kampuni ya
simu isipokuwa vifaa vya ujenzi wa minara ya simu.
Pamoja na
marekebisho hayo muswada huo unapendekeza kuongeza kifungu cha 3(d) ili
mtu yoyote asiruhusiwe kutoa misamaha ya kodi kwa miradi nayohusu
upanuzi na ukarabati wa miradi inayofanywa na wawekezaji.
Aidha
ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji baridi (soda) pamoja na kwenye maji ya
matunda (juice), iliyotengezwa kwa matunda yanayozalishwa hapa nchini
utabaki kama ulivyo sasa ili kuimarisha viwanda vya ndani.
Mkuya
alisema vinywaji baridi vimefanyiwa marekebisho ambapo ushuru kwenye
vinywaji hivyo utapunguzwa kutoka Sh 91 kwa lita hadi Sh 55 kwa lita.
Chanzo:Mwananchi
Post a Comment